Friday, December 16, 2011

KUZALIWA KWA YESU MASIHI

KUZALIWA KWA YESU KRISTO

Somo la 18 Luka 1 na 2

Matukio yahusianayo na kuzaliwa kwa Yesu Kristo yameandikwa katika kumbukumbu mbili za Injili. Yanapatikana katika Mathayo 1 na 2 na katika Luka 1 na 2. Luka atwambia kwamba matukio haya yalitokea katika utawala wa Kaizari Augustus (Luka 2:1-2), ambayo inatuwezesha kuthibitisha kwa usahihi kuwa Yesu alizaliwa mwaka wa nne kabla ya Kristo. Injili ya Luka pia imeweka kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji, na kujitokeza kwake katika taifa, ikiweka jambo hili katika sura ya ki-historia pia (Luka 3:1)
Tunapotafakari matukio haya tunafurahishwa na habari kamili zinazotokana na manabii wanaotabiri makusudi ya Mungu ya kumleta Yesu na kazi ambayo angefanya.

Unabii wa Isaya kuhusu kuzaliwa kwa Yesu

Isaya ndiye nabii aliyepeleka ujumbe dhahiri kwa nyumba ya Daudi akisema “Tazama bikira atashika mimba na kuzaa mwana ambaye ataitwa Immanueli (maana yake, ‘Mungu yu nasi’)” (Isaya 7:14). Hili lilitimizwa mara Mariamu, wa ukoo wa Mfalme Daudi alipomzaa mwanawe kifungua mimba Yesu kama alivyotabiriwa katika Mathayo 1:21-23.
Pia Isaya alitabiri kazi ya baadaye ya huyu ambaye angezaliwa akisema: “Kwa maana mtoto amezaliwa kwetu, kuna mwana ambaye tumepewa, na ufalme utakuwa begani kwake. _ _ _ _ kuhusu utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho, kwenye kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake ili kuufanya imara na kuutegemeza kwa njia haki na kwa njia ya uadilifu kuanzia sasa hata milele” Isaya 9:6-7). Kutokana na utabiri huu hatuwezi kushindwa kuelewa kuwa yesu alizaliwa ili atawale katika kiti cha Daudi wakati ufalme wake utakaposimikwa duniani, milele.

Ujumbe wa Malaika Gabrieli kwa Mariamu.

Malaika Gabrieli alipomtokea Mariamu, alimwambia kuhusu kazi maalum ambayo Yesu angefanya. Maneno yake yanamtambulisha Yesu kama uzao wa Daudi uliotabiriwa katika 2 Samweli 7:12-16: “Na tazama utashika mimba na kuzaa mtoto wa kiume ambaye utamwita YESU. Atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu Zaidi: na Bwana Mungu atampa kiti cha Enzi cha Daudi, baba yake: na atatwala juu ya nyumba ya Yakobo, milele na kuhusu utawala wake hakutakuwa na mwisho (Luka 1:31-33).
Tutafakari maana ya ujumbe wa Malaika Gabrieli kwa Mariamu.
“Utamwita YESU”, Neno Yesu katika Kigiriki ni sawa na neno Yoshua linalopatikana katika Agano la Kale ambalo maana yake ni “Yah (Mungu) ataokoa.” Kupitia Yesu Mungu alikuwa analeta uokovu kutoka kwenye dhambi na mauti kwa watu wote (Linganisha na Mathayo 1:21)
“ataitwa Mwana wa Aliye Juu Zaidi.” Angekuja kuwa “Mwana wa Mungu” aliyeahidiwa kwa Daudi katika 2 Samweli 7:14 (linganisha na Waebrania 1:5; Zaburi 2:7.
“Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.” Yesu ni “mzao” au mjukuu aliyeahidiwa kwa Daudi ambaye ataanzisha upya kiti cha enzi na ufalme wa Daudi duniani (2 Samweli 7:12-16; linganisha Isaya 9:6-7)
“Kuhusu ufalme wake hakutakuwa na mwisho” ufalme wake hautakuwa na mwisho kwa sababu Yesu Kristo ambaye atkuwa mfalme hafi (2 Samweli 7:16, Danieli 2:44, Ufunuo 11:15).
Katika mbiu fupi ya Malaika Gabrieli tunapata maelezo dhahiri ya kazi itakayofanywa na mtoto huyu ambaye alikuwa karibu kuzaliwa:
 Angewaokoa binadamu katika dhambi na mauti
 Angekuwa Mwana wa Mungu
 Angekuwa mwana wa Daudi, na kwa hiyo
o Angekalia kiti cha enzi cha Daudi
o Angetawala Waisraeli waliojikusanya upya
o Angeanzisha ufalme wa Mungu usio na mwisho duniani.

Jibu la Mariamu kwa mbiu ya Gabrieli lilikuwa la unyenyekevu na ukunjufu kwa matakwa ya Mungu. Aliuliza: “Hili litakuwaje? Maana simjui mwanaume?
Jibu la Gabrieli likawa; “Roho Mtakatifu atakujia na uwezo wa Aliye Juu Zaidi utakufunika: kwa hiyo hicho kitu kitakatifu kitakachozaliwa na wewe kitaitwa Mwana wa Mungu” Luka 1:34). Kupitia uwezo wa Roho Takatifu ya Mungu mtoto huyu angezaliwa na kuitwa “Mwana wa Mungu” kwa utimizo wa unabii wa Agano la kale (2 Samweli 7:14, Zaburi 2:7, angalia Matendo 13:32-33, Mwanzo 3:15).

Kuzaliwa Kwake Bethlehemu

Kuzaliwa kwa Yesu Bethlehemu kulikuwa kumetabiriwa na Nabii Micah (Micah 5:1-2) lakini Yusufu na Mariamu waliishi Nazareti kilometa 110 kaskazini mwa Bethlehemu. Mariamu alikuwa amekaribia kujifungua na katika hali ya kawaida ya kibinadamu ilionekana kwamba angejifungulia Nazareti. Walakini tunaona mkono wa Mungu ukifanya kazi miongoni mwa binadamu, kuonyesha makusudi yake (angalia danieli 4:17), kwa maana wakati huu Kaizari Augustus alitoa amri kwamba dunia nzima ilipe kodi (yaani watu wote waorodheshwe). Hili lililazimu Yusufu na Mariamu wafanye safari ndefu kwenda kwa mji wa babu zao, Bethlehemu kwa madhumuni hayo (Luka 2:1-6) kilichoonekana kama uamuzi wa mbali wa mtawala wa Kipagani, kilikuwa kwa kweli kimeongozwa na mkono wa Mungu katika mashauri ya wanadamu kwa maana Yesu alikuwa azaliwe Bethlehemu (Luka 2:4-7, Mathayo 2:4-6). Pia Micah alitabiri kazi ya baadaye ya Yesu akisema angekuwa “Mtawala Israeli” Hili litatimizwa mpaka mpaka atakaporudi kuja kusimika ufalme wa Mungu duniani.

Habari zenye kufurahisha za kuzaliwa kwake.

Tukio hili lililosubiriwa kwa muda mrefu na vizazi na vizazi vya wacha Mungu wa kuume na kike liltangazwa na malaika kwa wachunga kondoo katika nyanda za Bethlehemu. “Msiogope; kwa maana, tazameni, nawaletea habari njema za furaha kuu kwa watu wote. Kwenu leo hii amezaliwa Mwokozi ambaye ni Kristo Bwana katika mji wa Daudi” (Luka 2:10-11).

Aya ya 10:
“Habari njema” Hii ni tafsiri ya neno lilelile ambalo mahali pengine limeandikwa “Injili”.
“Kwa watu wote” Habari njema inayohusiana na Yesu Kristo Bwana si kwa Wayahudi peke yao bali kwa watu wote, Wayahudi na watu wa mataifa sawia. Hizi habari njema ni mbiu ya uwokovu ambao Mungu ametoa kupitia kwake (Marko 16:15-16, Wagalatia 3:26-27)

Aya ya 11:
“Katika mji wa Daudi” Ndiyo kusema Bethlehemu, mji alipozaliwa Daudi (1 Samueli 16:1) Israeli ilitarajia mtawala ajaye atokee katika mji huu (Micah 5:1-2).
“Mkombozi” Mwanadamu ni mwenye mauti na dhambi na anahitaji kukombolewa kutoka katika kifo. Kupitia kwa Yesu Kristo Mungu ametupatia msamaha wa dhambi na matumaini ya kuchangia kutokufa na kristo wakati atakaporudi duniani (2 Timoteo 1:10; 1 Wakorinto 15:21-23, 51-54) kwa hiyo Yesu ni “Ukombozi wa mwanadamu utokao kwa Mungu.”

Wanajimu Kutoka Mashariki.

Miongoni mwa wale waliokuwa wamesoma unabii na kutarajia kuzaliwa kwa Kristo wakati huo ni “Wanajimu kutoka sehemu za Mashariki.” Mara tu walipofika Yerusalemu walianza kuuliza. “Yuko wapi yule aliyezaliwa akiwa mfalme wa Wayahudi?” (Math. 2:2) walielewa kutokana na Manabii kuwa hatima ya mtoto aliyezaliwa ni kuwa Mfalme wa Wayahudi akikalia kiti cha enzi cha Daudi (2 Samweli 7:12-14; Isaya 9:6-7)
Herode aliposikia udadisi wa Wanajimu alifadhaika na kuita Makuhani na Waandishi na “kuwataka wamwambie ni wapi Kristo alipokuwa amezaliwa” (Math. 2:4), walijua jibu mara moja kutokana na Nabii Micah wakamjibu: katika Bethlehemu ya Yuda (Micah 5:2; Math. 2:5-6).
Kutokana na hili twaona kuwa Wayahudi walifahamu kwamba:
 Kristo angezaliwa
 Katika Bethlehemu
 Na angetawala “watu wangu Israeli.”

Yesu Mwana wa Mungu na Mwana wa Binadamu.

Majina haya mawili, “mwana wa Mungu” na “Mwana wa Binadamu” yanatumika katika kumbukumbu zote za Injili. Yanaonyesha kuwa Mungu alikuwa baba yake na wakati huo huo akiwa mzao wa Adam alihusiana na mwanadamu ambaye yeye alikuja kuokoa. Tunaona hizi nasaha mbili zikitangazwa na Gabrieli katika maneno yake kwa Mariamu. Angekuja kuwa “Mwana wa Aliye Juu Zaidi” yaani wa Mungu na angekalia “kiti cha enzi cha Daudi, baba yake” (Luka 1:32; 2 Samweli 7:12-14; Matendo 2:30).
Paulo asema “Wakati ulipotimia “Mungu alimtuma mwanaye aliyezaliwa na mwanamke katika sheria” (Wagalatia 4:4) kuhusu mwanae Mungu aliweza kusema “Wewe ni mwanangu, leo hii nimekuzaa” (Zaburi 2:7, Waebrania 1:5; 5:5)
Ingawa kuzaliwa kwa Yesu kulibashiriwa muda mrefu na manabii kuwepo kwake kulianza mara Mungu kupitia Roho Yake Takatifu aliposababisha Mariamu kubeba mimba, miaka 2000 iliyopita (Luka 1:35)
Nabii Isaya anataja kuzaliwa kwa Yesu Kristo Bwana kwa jinsi hii: “Na yeye (mungu) aliona kuwa hapakuwa na yeyote, na kuwaza kwamba hapakuwa na mtetezi: kwa hiyo mkono wake ukaleta uwokovu kwake” (Isaya 59:16).

Mungu kwa kuona hali ya dhambi za binadamu na kwa kujua kwamba hapakuwa na yeyote ambaye angeonyesha utii mkamilifu au kumwokoa mwanadamu katika utumwa wa dhambi na mauti, alichukua hatua ya kumpata mtu ambaye kwa kupitia kwake angeleta uokovu. Alimtia nguvu huyo aliyezaliwa na mwanadamu ili ashinde dhambi na mauti na hiyo kufungua njia ya wokovu na uhai kwake mwenyewe na wengine wote ambao wangekuja kwa mungu kupitia kwake, “ kazi ya mwana wa Adamu imeainishwa katika Waebrania 2:6-18.

Ulazima wa mungu kujihusisha na wokovu wa mwanadamu kutoka katika dhambi ulitabiriwa tangu mwanzo, Aliposema “uzao wa mwanamke” ungekiponda kichwa cha “nyoka” kuonyesha kwamba Mungu angemfunika mwanamke kwa kivuli chake ili azae mwana ambaye angevunja nguvu ya dhambi ya nyoka Mwanzo 3:15; Waebrania 2:14, Wagalatia 4:4)

Uhusianao wa Yesu na Baba yake.

Yesu, kwa uangalifu aliueleza uhusiano wake na Baba yake, kila mara akitambua udogo wake kwake katika kila jambo, yesu alisema: “Baba yangu ni mkuu kuliko mimi” “Yoh.14:28 linganisha na Yoh 5:19, 30). Uhusiano huu wa Baba na Mwana ulionyesha umoja au mwafaka katika makusudio yao (Yoh 10:30) Alikuja kutekeleza matakwa ya Baba yake Yoh 5:30; Waeb 10:7) na kwa njia ya kupendeza alionyesha tabia ya Baba (Yoh 14:9)

Uhusiano huu mkuu ulieleweka wazi na kwanza kabisa kuandikwa akiwa na umri wa miaka 12: “Hamjui kwamba ni lazima niwe katika nyumba ya Baba yangu?” Alitambua kuwa Baba yake alikuwa amemlea kwa ajili ya kazi maalum na alikuwa amedhamiria kuifanya. Maisha yake yalikuwa ya kujitoa na utii kwa Baba yake, yakuishia katika mateso na kifo msalabani ambapo watu wangekombolewa katika dhambi na mauti.

Katika uhai wake wote aliweza kusema “Chakula changu ni mimi kufanya mapenzi yake aliyenituma na kumaliza (Yoh 4:34) Na hivyo katika zile saa za mateso kuelekea kutundikwa kwake msalabani aliomba apate nguvu katika bustani ya Gelsemane kwa maneno haya: Baba kama inawezekana, naomba kikombe hiki kinipite; hata hivyo sikulingana na mapenzi yangu lakini kulingana na mapenzi yako. “(Mathayo 26:39) mapenzi ya Baba yake yalikuwa na nguvu zaidi na ilibidi yatimizwe. Mateso yake ya kutisha msalabani yalipokwisha alipaza sauti kwa kuridhika na afueni: “Imekwisha “akainamisha kichwa na kukata roho akijua kuwa kazi yake ilikuwa imekamilishwa (Yoh 19:30) Aliweza kusema “Nimemaliza kazi uliyonipa kufanya” (Yoh 17:4).

Tunapotafakari mapenzi na utii ambao mwana alimfanyia Baba yake wakati wote tunaweza kuelewa kwa nini mungu alibainisha mara mbili: “Huyu ni mwanangu nimpendaye nipendezwaye naye” (Math. 3:17, 17:5)

Kwa heshima, tuelewe kwamba, Yesu, japo mwanaume aliyezaliwa na hulka ya kibinadamu alikuwa pia mwana wa Mungu, ambaye kwa kushinda dhambi na mauti alifufuliwa katika wafu na kupazwa mbinguni na kukalishwa upande wa kulia wa Baba yake.

Ni muhimu kwamba tunaelewa wazi uhusiano wa Baba na Mwanae ili kuifahamu kazi ya Yesu Kristo Bwana wetu. Kukosa kuelewa kumesababisha dhana potofu ya utatu kwamba yesu alikuwa mungu, sawa na wa milele kama Baba. Fundisho kama hilo halipatikani mahali popote katika Biblia, Kuwa ushahidi wa kutosha kabisa kuthibitisha kuwa fundisho hilo ambalo limekuja kuwa la msingi kwa imani za kikristo siku hizi halikuundwa hadi miaka 300 baada ya Kristo.

Maneno yanayotumiwa kwa kawaida na wale wanaoshikilia fundisho la utatu kama, Mungu Mwana “aliyesawa” na mwenye “umilele” na hata Utatu”, hayapatikani mahali popote katika Biblia. Hata wafuasi wa kanisa wanaoheshimika wanatambua kuwa fundisho hilo halimo katika Biblia, lilijengwa kama fundisho la lazima na watu walioongozwa na falsafa ya Kigiriki na kulishushia kwenye mafundisho rahisi ya Biblia. Kwa kuwa inakubalika kuwa hakiwezikueleweka kinaitwa “fumbo”, Na hili limewavunja wengi moyo wa kutafuta ukweli.

Yesu mwenyewe, kwa upande mwingine alisema ni suala la uzima wa milele kumjua Mungu: “Uzima wa milele ndio huu, waendelee kupata ujuzi juu yako wewe, Mungu wa pekee wa kweli na yule uliyemtuma Yesu Kristo (Yohana 17:3).

Mtume Paulo anaandika juu ya jambo hili kwa uwazi kabisa: kuma Mungu mmoja na mtetezi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, Yesu Kristo (I Timotheo 2:5).


Yesu – neno lililogeuzwa kuwa Mtu

Mungu alimtangazia Musa na wana wa Israeli “Nitawainulia nabii kutoka katikati ya ndugu zao kama wewe; nami nitaweka maneno yangu katika kinywa chake, naye atawaambia maneno yote nitakayomwamuru na itatukia kwamba mtu ambaye hatasikiliza maneno yangu ambayo atayasema kwa jina langu mimi mwenyewe nitamtaka ajibu” (kumbukumbu 18:18 – 19, Hapa Mungu anatueleza mapema jinsi atakavyo ingilia kati masuala ya duniani na kumuinua mwana ambaye atamwagiza kunena maneno yake kwa taifa. Kwa kuwa aya hizi zimo katika mfumo wa wakati ujao Yesu, japo alikuwa katika mpango wa Mungu, hakuwepo wakati huo. Kwa kuwa Mungu alimuamuru mwanae kuweka maneno kinywani mwake, Yesu, pia aliitwa “Neno lililofanywa Mtu.
Tunasoma: “Neno lilifanywa Mtu na kuishi miongoni mwetu (na tuliona utukufu wake, utukufu kama wa mwana wa pekee wa Baba) uliojaa neema na ukweli” Yoh.1:14). Neno la Mungu halikuwa jambo la kinadharia tu bali lilokuwa na mwongozo wa kimaadili kwake ili kwamba alionyesha tabia halisi ya Baba yake akiwa amejaa neema na kweli. Hivyo yesu aliweza kumwambia Filipo; “yule aliyeniona mimi amemwana Baba na wewe utasemaje tuonyeshe baba yako?” Yoh. 14:9) Yesu hasemi kuwa yeye ndiye Baba, Anachosema ni “Ninafanya kile Mungu alichotaka nifanye na nina sema kile ambacho mungu amenitaka niseme kama umeniangalia utakuwa umeona kuwa ninewaonyesha tabia ya Baba yangu kwa sababau mimi ni mwanawe na siku zote ninatekeleza mapenzi yake” kabla ya kusulubiwa alimwomba Baba yake akisema “Nimelitambulisha jina lako kwa watu ulionipa duniani” (Yoh. 17:6)

Kila mara Yesu alikiri kuwa maneno aliyo kuwa akisema hayakuwa yake mwenyewe bali aliyofundishwa na Mungu: Sijajisemea Mwenyewe; bali Baba aliyenitumia akinipa amri, ninachotakiwa kusema na ninachopaswa kunena. Na ninajua kuwa amri yake ni uzima wa millele. Chochote ninachosema kwa hiyo ni kile Baba alichoniambia kwa hiyo ninasema (Yoh 12:49-50, 7:17, 8:28) Yesu alisisitiza siku zote kuwa alikuwa Mwana wa Mungu na mdogo kwa Baba yake.
Alisisitiza hivi: “Baba yangu ni Mkuu zaidi kuliko mimi” (Yoh.14:28) Wayahudi waliposema Yesu “anajifanya kuwa hawezi kufanya lolote peke yake,” na tena “Mimi peke yangu siwezi kufanya chochote” Yoh 5:18 – 19, 30)

Uhusiano huu mzuri kati ya Mungu na Mwanae ni wa msingi kueleweka kama tunataka kuamini ukweli. Yesu alisema “Huu ni uzima wa milele kwamba waweze kukujua wewe Mungu pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma (Yoh. 17:3)


Maisha ya Yesu ya awali

Kumbukumbu za injili za twambia machache sana kuhusu maisha ya yesu kwanzia alipozaliwa hadi alipofikisha umri wa miaka 30, wakati alipotambulishwa katika taifa lake kwenye ubatizo wake na Yohana Mbatizaji (Luka 3:23)

Tukio peke yake lililoandikwa ni pale alipoandamana na Yusuf na Mariamu kwenda Yerusalemu kwenye sikukuu ya Pasaka alipokuwa na umri wa miaka 12, hapa tunasoma: “Yesu aliongezeka katika hekima na urefu na katika kupendwa na Mungu pamoja na wanadamu” (Luka 2:41 – 52)


MUHTASARI

 Kuzaliwa kwa Kristo kulikuwa kumetabiriwa na Nabii Isaya (Isaya 7:14; 9:6–7).
 Neno “Yesu” maana yake ni “Mungu (Yah) ataokoa”. Ni Mungu ndiye aliyemtoa Mwanae kwa wokovu wa Wanadamu katika dhambi na mauti (Math 1:21, linganisha na Isaya 45:21 – 22).
 Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu na kumwambia kuwa angezaa mwana wa Mungu ambaye pia Mwana wa Daudi (Luka 1:31 – 33; 2 Samweli 7:12 – 14).
 Yesu alizaliwa akiwa yule aliyeahidiwa kukaa kwenye kiti cha Daudi, Yerusalemu mara kitakaporudishwa na atatawala milele (Luka 1:31 – 33, 2 Samweli 7:12 – 16).
 Bethlehemu ni mji ule ambapo Yesu angezaliwa (Micah 5:2, linganisha na Math 2:4 – 6, Luka 2:4 – 11 )
 Tabia ya Mungu ilidhihirishwa katika maisha ya Mwanae (Yoh 14:9,17:6) kwa kuwa siku zote alinena maneno ya Mungu aliitwa Neno lililofanywa mtu Yoh 1:14, Kumbukumbu 18:18 – 19; Yoh 12:49 – 50; 7:17; 8:28)
 Yesu ana tajwa kama “Mwana wa Mungu” Hakuna mahala popote katika Biblia alipotajwa kama “Mungu Mwana” wala hadai kuwa sawa na Mungu au wa milele na Mungu kama mafunzo ya utatu yanavyodai, Siku zote alikiri kuwa Baba yake alikuwa Mkuu kuliko yeye, (Yoh 14:28 Linganisha na 5:18 – 19, 30)

SOMO LA 18 – MASWALI

1. Jina “Yesu” lina maana gani?
2. Maneno ya Malaika Gabrieli yalibashiri nini kuhusu kazi ya Yesu Kristo?
3. Maneno haya yatatimizwa lini?
4. Yesu alizaliwa katika mji gani wa Israeli?
5. Kwa nini Yesu anaitwa Mwana wa Binadamu?
6. Mungu alimsema Yesu “Nitakuwa Baba yake nae atakuwa Mwanangu” (2 Samweli 7:12 – 14 na Waebrania 1:5) Je Yesu alikuwepo kabla ya kuzaliwa na Mariamu huko Bethlehemu?
7. Je Yesu alidhihirishaje Jina la Mungu katika maisha yake?
8. Yesu hakudai kuwa sawa na Mungu katika maisha yake. Nukuu kifungu kinacho sema Baba yake ni Mkuu kuliko yeye.

Tuesday, January 4, 2011

WAS MUHAMMAD SURE OF HIS DESTINY?!

Mohammad was not sure about his destination:
Mohammad Wasn't Sure about his destination while all the Bible prophets were surely knew that they were going to heaven after death.
Jabir reported that the Prophet of Islam said: "No good works of yours can ever secure heaven for you, nor can they save you from hell -- not even me, without the grace of God."
Abu Huraira related that when the verse, "Cause thy near relatives to fear," was revealed to the Prophet of Islam, the Prophet arose and began to proclaim: "Oh people of the Quraysh, and you sons of Abdul Manaf, and you Abbas, son of Abdul Muttalib, and you, Safiyyah my aunt, I cannot save you from the punishment of the Day of Resurrection. Take care of yourself, O my daughter Fatimah; you may use my property, but I cannot save you from God. Take care of yourself" (Bukhari).
Abu Huraira reported that the Prophet of Islam said: "No one of you will enter Paradise through his good works." They said: "Not even you, O Apostle of God?" "Not even I," he replied, "unless God cover me with His grace and mercy. Therefore be strong, and morning and evening, nay every moment, try to do good."
Mohmmad's prayer asking forgiveness:
Volume 1, Book 12, Number 711:
Narrated Abu Huraira:
Allah's Apostle used to keep silent between the Takbir and the recitation of Qur'an and that interval of silence used to be a short one. I said to the Prophet "May my parents be sacrificed for you! What do you say in the pause between Takbir and recitation?" The Prophet said, "I say, 'Allahumma, ba'id baini wa baina khatayaya kama ba'adta baina-l-mashriqi wa-l-maghrib. Allahumma, naqqim min khatayaya kama yunaqqa-ththawbu-l-abyadu mina-ddanas. Allahumma, ighsil khatayaya bil-ma'i wa-th-thalji wal-barad (O Allah! Set me apart from my sins (faults) as the East and West are set apart from each other and clean me from sins as a white garment is cleaned of dirt (after thorough washing). O Allah! Wash off my sins with water, snow and hail.)"
is Heaven promised in Islam?
Allah Promised hell for his followers:
Al-Imran (The Family of Imran)
Sura 3:185, "Every soul shall have a taste of death: And only on the Day of Judgment shall you be paid your full recompense. Only he who is saved far from the Fire and admitted to the Garden will have attained the object (of Life): For the life of this world is but goods and chattels of deception."
This Suras from Quran very clearly says that after death everyone will go to hell fire then judgment.. When a person went to hell fire then how and why it is possible that he/she can come out from hell fire and go to paradise.. no way.. This verse does not say anything about eternal life. This verse very clearly says that every believer in Allah is tasting death means they did not get the life while Jesus promised eternal life and heaven as we read in
John 10:10 "The thief does not come except to steal, and to kill, and to destroy. I have come that they may have life, and that they may have it more abundantly.
And also every soul is going to hell fire till the day of judgment means they are not reaching heaven. So of course Allah promised hell fire for his believers. I said "no way" for coming out from the hell fire and go to heaven. There is no chance to go to heaven once you go to hell fire... But yes, Jesus can save you when you are still in this world as He said in John 3:15 "that whoever believes in Him should not perish but have eternal life.
John 3:16 "For God so loved the world that He gave His only begotten Son, that whoever believes in Him should not perish but have everlasting life.

How a person can save himself/herself from hell fire when he/she is already in hell fire? And this verse says that they will be there till the time of Day of Judgment. Do you think a person who is already in hell fire will get a seat in heaven after judgment? Judgment is a day when people get their sentence and verdict.. no reward my friend that day.
Allah promised hell fire for his followers but contrary to it Jesus promised heaven for His followers.


Mohammed foretold destination - Hell
The greatest difference between Allah and Elohim is that Allah promised hell fire and torture for his follower while Elohim promised heaven and eternal life for his followers! Mohammed could portrait and visualize it while he was in this world as we read in this Hadith:
Volume 1, Book 12, Number 770:
Narrated Abu Huraira:
The people said, "O Allah's Apostle! Shall we see our Lord on the Day of Resurrection?" He replied, "Do you have any doubt in seeing the full moon on a clear (not cloudy) night?" They replied, "No, O Allah's Apostle!" He said, "Do you have any doubt in seeing the sun when there are no clouds?" They replied in the negative. He said, "You will see Allah (your Lord) in the same way. On the Day of Resurrection, people will be gathered and He will order the people to follow what they used to worship. So some of them will follow the sun, some will follow the moon, and some will follow other deities; and only this nation (Muslims) will be left with its hypocrites. Allah will come to them and say, 'I am Your Lord.' They will say, 'We shall stay in this place till our Lord comes to us and when our Lord will come, we will recognize Him. Then Allah will come to them again and say, 'I am your Lord.' They will say, 'You are our Lord.' Allah will call them, and As-Sirat (a bridge) will be laid across Hell and I (Muhammad) shall be the first amongst the Apostles to cross it with my followers. Nobody except the Apostles will then be able to speak and they will be saying then, 'O Allah! Save us. O Allah Save us.'

There will be hooks like the thorns of Sa'dan in Hell. Have you seen the thorns of Sa'dan?" The people said, "Yes." He said, "These hooks will be like the thorns of Sa'dan but nobody except Allah knows their greatness in size and these will entangle the people according to their deeds; some of them will fall and stay in Hell forever; others will receive punishment (torn into small pieces) and will get out of Hell, till when Allah intends mercy on whomever He likes amongst the people of Hell, He will order the angels to take out of Hell those who worshipped none but Him alone. The angels will take them out by recognizing them from the traces of prostrations, for Allah has forbidden the (Hell) fire to eat away those traces. So they will come out of the Fire, it will eat away from the whole of the human body except the marks of the prostrations. At that time they will come out of the Fire as mere skeletons. The Water of Life will be poured on them and as a result they will grow like the seeds growing on the bank of flowing water......
Let us analyze this Hadith and see what does it say?
This Hadith says that Mohammed is not in heaven right now but he is waiting for the 'Day of Judgment' to go into heaven and he will be the first to cross the bridge to go to heaven as we read this, "Then Allah will come to them again and say, 'I am your Lord.' They will say, 'You are our Lord.' Allah will call them, and As-Sirat (a bridge) will be laid across Hell and I (Muhammad) shall be the first amongst the Apostles to cross it with my followers. Nobody except the Apostles will then be able to speak and they will be saying then, 'O Allah! Save us. O Allah Save us.' "
Hadith Volume 1, Book 8, Number 345 also says that while Mohammed was in this world he ascended into heaven and saw many prophets and other Bible characters like Adam, Moses, Jesus and Abraham. And he saw the paradise while he was still alive and on this earth but why he should wait to go to heaven after his death? I asked many Muslims where Mohammed is right now and why he is waiting for the 'Day of Judgment? Why he could not reach heaven while he saw many ancient prophets and the first human of this planet earth - Adam who lived many thousands of years before Mohammed. All are in heaven but Mohammed says, he will reach heaven on the Day of Judgment, why? But no Muslim could reply these questions.
Yes, my friend, death is not the end of your life. There is a life after death and the God of the Bible promised heaven for those whose sins are forgiven. All the Bible prophets were dead sure that they are going to heaven after death but Mohammed was not. It is because Allah does not promise eternal life for anybody. The Hadith further says that Mohammed will say, 'O Allah! Save us. O Allah Save us.' But the Bible says that there is no hope after death for our salvation. We have to get salvation in this world itself as we read in Isaiah 38:17-18, "Indeed it was for my own peace That I had great bitterness; But You have lovingly delivered my soul from the pit of corruption, For You have cast all my sins behind Your back. For Sheol cannot thank You, Death cannot praise You; Those who go down to the pit cannot hope for Your truth.
When David sinned against God, he asked God to restore the joy of salvation as we read in Psalms 51:12, "Restore to me the joy of Your salvation, And uphold me by Your generous Spirit."
David was saved when he was in this world itself. Isaiah got the forgiveness of his sins while he was in this world itself. So Bible makes it clear that we have to get saved in this world itself and that after death there is no hope to know God or to get salvation.
The same Hadith that I quoted above says this, "He will order the angels to take out of Hell those who worshipped none but Him alone. The angels will take them out by recognizing them from the traces of prostrations, for Allah has forbidden the (Hell) fire to eat away those traces. So they will come out of the Fire, it will eat away the whole of the human body except the marks of the prostrations. At that time they will come out of the Fire as mere skeletons. The Water of Life will be poured on them and as a result they will grow like the seeds growing on the bank of flowing water....."
This Hadith clearly says that the followers of Allah are going straight to hell fire as this Hadith says that Allah will order the angels to take out of Hell those who worshipped none but Allah alone. And angels will recognize them by the marks of prostrations.
But how sad it is that Muslims are waiting to go to this horrible place. How sad it is that they are following a god who promised hell fire for them. How sad it is that they put all their trust and belief on Allah with all their heart and with all their passion just to go to Hell fire! But no, there is a way out, there is a God who gives eternal life and heaven to His followers whose name is Jesus. Jesus said in John 5:24 "Most assuredly, I say to you, he who hears My word and believes in Him who sent Me has everlasting life, and shall not come into judgment, but has passed from death into life.
Yes, after death there is no chance to come out of hell fire but you can have assurance of heaven in this world itself through Jesus. Further this Hadith says, "So they will come out of the Fire, it will eat away from the whole of the human body except the marks of the prostrations. At that time they will come out of the Fire as mere skeletons. The Water of Life will be poured on them and as a result they will grow like the seeds growing on the bank of flowing water"
But this is not true saying! Jesus came to give the "living water" or 'Water of Life' while we are in this world itself. Jesus said to the Samaritan woman in John 4:10, "If you knew the gift of God, and who it is who says to you, 'Give Me a drink,' you would have asked Him, and He would have given you living water."
We can receive this living water i.e. Holy Spirit in this world itself. When Jesus was about to go from this world He promised to send His Holy Spirit and He fulfilled His promise. After 50 days of His ascension to heaven He sent His Holy Spirit and filled them. (Acts 2:4) And Jesus also said in John 7:38 "He who believes in Me, as the Scripture has said, out of his heart will flow rivers of living water."
Yes, my friend, you need not to wait till the 'Day of Judgment' and after being removed from hell fire as the Hadith says, but living water is available freely for you when you are still in this world. You can receive this living water and live forever and forever in heaven!
So we can clearly draw a line between Allah and Elohim and we can say that Allah and Elohim are not same God but opposite to each other. If they are the same God then why did they promise two different things? Both of them should have promised heaven and eternal life. But we can see that Allah promised hell fire and eternal doom for his followers but Elohim/Yahweh/Jesus promised heaven and eternal life for His followers!
If you want this eternal life and if you want to go to heaven please pray this prayer with me:
Loving Jesus, I am a sinner and I know that by my own efforts I can not achieve forgiveness of my sins or salvation. Please save me from my sins and hell fire and please give me eternal life so that I may never go into hell fire but have eternal life and live in peace and joy with you. Please save me Lord. I confess all my sins before you and I invite you to come into my life. Please come into my life and give me assurance of heaven. Thank you for listening to my prayers. I give you all the glory. I pray in the mighty name of Jesus, Amen.

HAKUNA MABADILIKO KATIKA MANENO YA ALLAH

HAKUNA MABADILIKO KATIKA MANENO YA ALLAH:

DIBAJI

Fikira na mawazo yetu ni kipaji kutoka kwa Mungu.lakini kwa kuwa mawazo yetu yana kikomo ni kosa kufikiri mawazo yetu yanaweza kufahamu yote kuhusu Mungu aliye mkuu.Msingi wa kitabu hiki kwa kuhusiana na imani ya kikristo ni kwamba Biblia ndiyo msingi wetu juu ya imani na matendo.

Kwa vile haja yakutafsiri kitabu hiki ilikuwa kubwa mno, niliombwa kufanya kazi hii nzito nami namshukuru Mungu kwa kuniwezesha.

Wayahudu kwa uangalifu mkubwa wameweza kuhifadhi maandiko yote katika lugha ya kiebrania na kiaramu hadi hivi leo.Wakristo tumekubali kupokea agano la kale kutoka mkononi mwa Wayahudi kwa mamlaka ya bwana Yesu Masihi mwenyewe.Vitabu vilivyopokelewa na Wakristo vilibakia vivyo hivyo kama vilivyokuwa wakati wa wayahudi waliokuwa wakiishi zamani za Masihi na vingali hivyo katika nchi zote hata hivi leo.

Sheikh Muhammad kamal anabainisha wazi ni kwa nini Wakristo hatuamini kuwa Bibilia imegeuzwa.Uamuzi huu si wa kihisia tu bali inatoa hoja thabiti inayotokana na Uchunguzi wa mambo kwa makini.Ni upuuzi kwa mtu yeyote kujidai kuwa anaweza kuelewa kila jambo kuhusu ufunuo wa mungu tuliopewa katika maandiko ya Biblia.Hata hivyo ninaamini hivi ni kuonyesha upungufu katika vitabu vilivyofunuliwa.

Ndugu yangu naamini utayathamini aliyoyaeleza humu, kuwa Biblia ni yenye kuaminika na kwamba utajisomea ushahidi uliomo.

Ni imani yangu kwamba,ewe ndugu yangu mwislamu utakaposoma kitabu hiki kwa makini na kwa moyo wa uwazi utaweza kutambua,kweli kwamba Biblia takatifu iliyo kusanya vitabu vya Taurati ,Zaburi na Injili na vitabu vya manabii wengine haijachafuliwa wala kuharibikacwala kufutwa aya zake.Bali Mungu anayelinda maneno yake na atayalinda daima dawamu kama alivyoahidi.

Asante nyingi kwa Sheikh Muhammad na hasa wote mlio kubali kusoma na kufanya masahihisho ya mwisho kabla ya kupiga chapa kwa tafsiri hii ya Kiswahili iliyofanywa nami Mwalimu Chaka wa Musa.














HAKUNA MABADILIKO KATIKA MANENO YA ALLAH:


Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.

Kwanza yanipasa nimshukuru Mola wetu mlezi ambaye ametupa uwezo wa kununa na kutumia karama ya fikra na kututenganisha na viumbe wengine wote. Baada ya kuipokea na kuikubali njia ya Bwana, na mwongozo wake, matokeo yake ni makuu na yametimizwa na ahadi ya uzima wa milele mbinguni. Kutakuwa na baraka tele na furaha kwani ALLAH amesema: ‘kwa wale wafuatao imani, kutakuwa na zawadi tele zaidi ya chochote chenye kufikiriwa, zaidi ya chochote kionekanacho au kinachosikika.’

Ebu tutumaini kuwa miongoni mwa hao watao bahatika.

Mola wetu aliyetupa akili timamu na fikra safi pia atatuongoza na kutuelekeza, kuona mwanga na kweli utakaotuongoza kwa usalama. Bwana uufanye mkono wetu unyoke kufikilia uwongofu.

Mungu mkuu amefanya tangazo hili:
“Msiliongeze neno niwaamuru wala msilipunguze, mpate
kusishika amri za BWANA, Mungu wenu mwaamuzi’ Kumb 4:2

Na mwishoni kwa injili tukufu, tunasoma onyo kali.

‘Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki,Mungu atamwondelea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.’ Ufunuo 22:18-19.

Baada ya amri hizi nzito namna hii, Je pana mtu yeyote mwaminifu atakayeleta changamoto kwa neno la Mungu au kulibadilisha neno la BWANA?

Imefikiriwa na baadhi ya Waisilamu wengi kwamba Biblia (Yaani Taurati, Zabur na Injili) imechafuliwa na kubadilishwa mara nyingi wakati tofauti tofauti , ima kwa kuongeza jambo ndani yake au kwa kuondoa jambo humo ndani. Kwa muda mrefu watu wenye mawazo haya wamejaribu kuleta hoja dhidi ya Biblia ijapo kwa kweli bado hawajafaulu kuleta ushindi kamilifu kwao basi ni wazi kwamba wamepoteza msingi wote kwa madai yao.


Ndungu yangu Muislamu,ni jambo la ajabu kwamba watu leo hii bado wangali wanadai kwamba Biblia (Taurati, Zaburi na Injili) imefanyiwa mabadiliko ambayo yanaleta utata kati ya Biblia halisi ya awali na Quran. Ni jambo lakusikitisha kwani Quran inashuhudia Biblia, kwamba Biblia kwa kweli ni maneno ya ALLAH, Yaliyoletwa na Mola wetu mwema kuwa nuru , muongozo na rehema. Biblia kwa kweli ni neno la ALLAH ambalo halijawahii kubadilishwa au kuletewa ushindani. Qurani inashuhudia ukweli huu, kwamba hapana mabadiliko katika maneno ya ALLAH.

Ushahidi wa kuunga mkono usahihi wa Biblia ni mwingi zaidi ya uvuli wowote wa shaka. Qurani inatupa ushahidi , Ndungu yangu Muislamu , unaushuhudia ukweli kwamba , Taurati ni kitabu kilicholetwa kutoka kwa Mola wetu mlezi kwa bwana wetu Musa, kuwa muongozo na rehema kwa walimwengu.

‘Hakika sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru…
Q 5:44

Ni wazi kuwa Taurati imetoka kwa BWANA:

‘Sema : Nani aliyoteremsha kitabu alicho kuja nacho Musa,
chenye nuru na uwongofu kwa watu.’ Q6:9


Pasi na shaka ni wazi kuwa Taurati tumepewa kutoka kwa BWANA wetu MLEZI. Mwenyezi .

‘Na hakika tulimpa Musa kitabu na tukafuatisha baada yake
Mitume wengine” Q 2:7

Ni vyema tukumbuke kwamba Taurati aliyokabitiwa Musa:imeitwa “kitabu”

‘Na tulipo mpa Musa kitabu na pambanuo (baina ya haki na
baatili) ili mpata kuongoka.’’ Q 2:53


Hapo pia pana kiashiria ina ukweli kwamba. Taurati alipewa Musa (kitabu na kipambanuzi) Al – Baidwawi anasema katika ufafanuzi wa aya hii:
(Yeye ni miongoni mwa wafafanuzi wazuri na wanaokubalika) kwamba pambanuo inamaanisha kwamba Taurati iljumuisha maana ya kitabu kilicho weka utofauti bayana baina ya halali na haramu, haki na baatili.

“Na kwa yaini tuliwapa Musa na Haaruni kipambanuzi na
mwangaza, na makumbusho kwa wachamungu” Q 21:48


Al – Baidwawi alisema katika ufafanuzi wake kwamba Taurati ni mwangaza, ni nuru ya kuwaongoza watu wafuate njia ya kheri kuwatoa kwenye kufa moyo na ujinga wa kutofahamu, kuwaongoza watu kwenye kweli ambao ndio utakaowaokoa.


MUKHUTASARI: Ni bayana kwetu , ndungu yangu Muislamu, kutokamana na ufafanuzi huu wote , kwamba Taurati ni kitabu alichopewa Musa na Mola mlezi kama mwongozo, nuru na rehema kwa ulimwengu. Kwa maana hiyo: kwa kuwa Taurati ililetwa na ALLAH.(Quran inapeana ushahidi wa kutosha). Basi ni wazi kuwa Taurati ni maneno ya ALLAH mtukufu.

“Na tulikwisha andika katika zaburi – nacho ni kitabu cha David baada ya Taurati kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema wapate kuitengeneza na kuusahilisha njia za maisha bora humo.”
(Bali wenye upole watairithi nchi.” Zaburi 37:11

wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele.” Zaburi 37:29


Na sasa kwako ndungu yangu Muislamu, huu hapa ushahidi wa Qurani, unaoshuhudia kwamba zaburi alipewa Nabii Daudi.


‘Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa zaburi.’ Q 17:55

“Na hakika tulikwisha andika katika zaburi baada ya kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.’’21:105



MUKHTASARI: Ni wazi sasa kwako ndungu yangu Muislamu, kwamba Mwenyezi Mungu amepeana Zaburi kwa mja wake Daudi na ALLAH ( Qurani inashuhudia jambo ili) hivyo basi Zaburi ni neno la ALLAH.


Sasa ndungu yangu Muislamu, ukweli huko bayana kwamba injili pia ililetwa kutoka kwa ALLAH wa Bwana wetu Isa Massihi kuwa nuru mwongozo na mfano kwa wachamungu.

‘Na wahukumu watu wa injili kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu ndani yake.’ Q 5: 47


Na huu ndiyo ushahidi wa ukweli kwamba kila kilichomo ndani ya injili kilipeanwa na Bwana wetu.


“ Na sisi tuliwaamrisha wafuasi wa Isa yaani . Watu wa injili , wakristo, wahukumu kwa hukumu alizo teremsha mwenyezi Mungu. Na wasio hukumu kwa musibu wa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu basi hao wameiacha sharia ya mwenyezi Mungu, ni waasi.”

“Amekuteremshia kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo)”



Kutokamana na ushahidi huu, ni bayana kuwa injili imetoka kwa Bwana kuongoza ulimwengu wote kama vile Qurani ilivyotambua Taurati na Biblia kuwa kipambanuzi. Ni vyema pia kutambua usawa uliopo baina ya Taurati , Injili na Quran


“Enyi watu wa kitabu, mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake” Q3: 65


Twaweza kuona kwa uhakika, jinsi gain ilivyo bayana kwamba Taurati na Injili zote zilipeanwa na ALLAH.


“Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati , na tukampa injili ilyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo. Sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamungui.’’ Q 5:46


Kwa mara nyingine tena, twaona kuwa injili aliyopatiwa kwa bwana wetu Isa iwe muongozo na nuru.



‘Tena tukafuatisha nyuma yao mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu, na wengine tukampa injili. Na tukajaalia katika nyoyo za waliomfuatia upole na rehema.”


Tena kwa mara nyingine Quran inatuakikishia kuwa injili imetolewa kwa Allah kwa Bwana wetu Issa


MUKHUTASARI: Kutokamana na haya yote, ni wazi kwetu sote ndungu yangu Muislamu, kwamba injili imepeanwa na ALLAH mtukufu, kwa bwana wetu Issa kama mwongozo na nuru ya ulimwengu . Na hivyo basi kwa kuwa injili ni kitabu kilichopeanwa na ALLAH.( Quran inashuhudia hili) hivyo basi injili ni neno la Allah.

Ndungu yangu Muislamu, hapa pia utapata ushahidi mwingi zaidi kuhusu uhalali na usafi wa Biblia Tkatifu ( Taurati, Zaburi na injili katika sehemu zake zote.

“Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.” Q 16:43

“ Tungependa tungeli wateremshia kutokamana na aya hizi mbili za Bwana wetu mlezi kwa yeyote yule muisilamu ni wazi kuwa:

1.Unabii wote kutoka kwa ALLAH ambao ulipewa kwa hao watu wa Mungu kabla ya Muhammad kwa kweli na bila shaka ulitoka kwake Allah. Mola wao. Zingatia neno,Kabla yako ewe Muhamad na vilevile neno ‘uliopewa wewe ewe Muhammad.

2.Kwa kuwa Musa na Daudi ni miongoni mwa manabii wakuu walioshi kabla ya Muhammad vitabu vyao vilitoka kwa Mola mlezi. Na kwa vile Musa alihubiri Taurati, Daudi Zaburi na Isa Injili , vitabu hivi vitatu vitakuwa vimetoka kwa ALLAH.

3. Neno “Alipewa” linammanisha kwamba yote waliyopewa yalikuwa ni maneno ya ALLAH kwa maana hiyo;Taurati Zaburi na Injili vyote ni maneno ya ALLAH mtukufu.


“Hakika sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Natulimpelekea wahyi Ibrahim na Ishmail na Is – haka, na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daudi tukampa Zaburi” Q 4 :163

Kutokamana na haya twaweza fikia hatima hii:

a. Maneno yaliyoshushwa kutoka kwa ALLAH kwa Muhamad yalikuwa sawa kama yale ya Nuhu na manabii wengine waliomfuata (kumbuka na zingatia neno uliyopewa ewe Muhammad)
b. Kwa vile Musa Daudi na Isa wote walikuja baada ya Nuhu, mafundisho yao yalitoka kwa Mola wao Mlezi .Ivyo pia vitabu vyao vyote (Taurati, Zaburi na Injili) yalitoka kwa Mola kulingana na uisilamu yalikuwa ni maneno ya ALLAH yaliyopewa kwa Musa , Daudi na Isa.


MUKHTASARI: Kutokamana na haya, ni wazi kwa Muisilamu yeyote kwamba Qurani kwa bayana inatangaza kwamba Biblia Takatifu (Taurati, Zaburi na Injili) imetoka kwa mwenyezi Mungu. Tazama (Q 26: 3:16:43, 4:163)


Ndungu yangu muisilamu haya ndiyo majina ya sifa ya Taurati na Injili kama yalivyotajwa ndani ya Qurani :

1. Qurani inavipa Taurati na Injili jina la “KITABU”

“Sema:Enyi watu wa kitabu! hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokamana na Mola wetu mlezi.” Q 5:68
“Ewe mtume! Waambie watu wa kitabu (yaani Biblia). Hakimka ninyi hamtakuwa mnafuata dini sahihi ila mtazitangaza hukumu zote za Qurani”
Q 25:63

“Wala msijadiliane na watu wa kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa.”Q 29:46


“Enyi mlio pewa kitabu ! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo” Q:4:47


“Watu wa kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Q 4 : 153

Kutokamana na haya twaona wazi kuwa Qurani inaipa Taurati na Injili neno ‘kitabu” ushahidi huu unaungwa mkono pale Qurani inapowatambua wayahudi na wakristo kama “Watu wa kitabu” neno ambalo limerejelewa mara 20 ndani ya Qurani.


2. Qurani inaipa Taurati na Injili sifa ya kuitwa “Dhikr”(Ujumbe wa Mungu)


“Na kabla yako hatukuwatuma watu ila wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui” Q 21:7


Nukuu hii imetajwa katika ufafanuzi wa AL-Jalaleen (uk357) akihitimiza kuwa Qurani inatambua Taurati na Injili kama ‘Al-Dhikir’


MUKHUTASARI: Maneno haya “kitabu” na “Al-Dhikir” ni majina ambayo pia Qurani inajitambua kwao.Kwa kuwa Qurani inaipa Biblia Takatifu jina lilelile lake, huu ni ushahidi tosha kwamba Taurati na Injili vimetoka kwa Bwana Mungu.


“Amekuteremshia kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyokuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili. Q 3:3


Haya yote yana dhihirisha wazi kuwa Qurani inatambua Taurati na Injili kuwa na uongozi , nuru, Rehema na Ufunuo.Qurani pia inatuhakikishia kuwa Taurati na Injili vimetoka kwa Mola wetu mlezi



UHAKIKA KUTOKA KWA QURANI:

1. Taurati, Zaburi na Injili vyote ni vitabu vya kibinguni tulivyo pewa na Mola wetu mlezi (Q5:46,17:55,3:3)
2. Taurati, Zaburi na Injili vyote ni sawa sawa na Qurani. (Q 16: 43, 4:163)
3. Qurani vilevile inatambuliwa kwa majina yaleyale ya Taurati na Injili (“kitabu” na “Al – Dhikir) Taz Q 21: 7, 20:99,113
4. Qurani inaelezea kuwa Taurati na injili ni vitabu vitakavyostahiki kuwa vitabu vya mwenyezi Mungu.

Kutokamana na haya yote, Ndungu yangu muisilamu, twaona wazi kuwa Qurani inanakiri kuwa Biblia Takatifu ( Taurati, Zaburi na Injili) ni maneno ya Mungu mkuu.

Huenda kweli utakubali kuwa Biblia Takatifu (Taurati,Zaburi na Injili) ni neno la Mola mlezi kwa kuwa Qurani inashuhudia jambo hilo. Lakini unaweza kusema kwamba baadaye imefanyiwa mageuzi na kubadilishwa. Pia waweza kuwa na fikira kama za ndungu zetu wengine kuwa kweli Taurati ni kitabu kilichotoka kwa Mola wetu kwa kuwa Qurani inashuhudia hilo, lakini Taurati ilifanyiwa mageuzi baada ya Musa na kwa sababu hiyo Mola wetu akampa Injili bwana wetu Isa mwana wa Mariamu. Hata hivyo watu hawa husema pia kwamba injili nayo imefanyiwa mageuzi na ndio maana Allah akaleta Qurani kuwa ukurasa wa Mwisho wa ufunuo wake.

Ebu nikwambie ndungu yangu muisilamu , kwamba Qurani yenyewe inashuhudia ukweli kwamba hapakuwa na mageuzi au mabadiliko yoyote katika maneno ya ALLAH baada ya kupitiwa Musa , Daudi na Isa.

“Hakika sisi ndio tulio teremsha ukumbusho huu na hakika sisi ndio tutaoulinda” Q 15:9

Nukuu hii inadhihirisha bayana kuwa Taurati na Injili vyote vimetoka kwa Allah na vimelindwa bila mabadiliko yoyote. Waweza ukadhani ndungu yangu muisillamu;kwamba Qurani ndiyo inayo ashiria kinapotajwa kitabu kitakatifu (Al – Dhikr) wala za Taurati na Injili. Lakini tukumbuke kuwa Qurani yenyewe ndio iliyo vipa kitabu hivi viwili sifa ya Al – Dhikr.”

“Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema” Q 21: 105

Ni wazi kwako sasa kwamba kitabu kitakatifu (Al – Dhikr) kinamaanisha Taurati na wala sio Qurani: ushahidi ukiwa kwamba Zaburi imekuja baada ya Taurati, wala sio baada ya Qurani.

“Na kabla yako hatukuwatuma watu ila wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui.” Q 21: 7


Wataalamu na wanavyioni akiwemo Al – Jalaleen (uk 357) na Ibn Kathir (uk 502) wanashikilia maoni kuwa watu waliotajwa katika Al – Dhikr ni wayahudi na wakristo. Sasa utakubaliana nami, ndungu yangu muisilamu, kwamba Taurati na Injili vimetolewa kwa Allah na vyote vimelindwa kutokamana na mageuzi na mabadiliko yoyote yale.

MUKHTASARI: Sote twatambua wazi kwamba Qurani inashuhudia ukweli kwamba hapajakuwa na mabadiliko katika maneno ya Allah na kwamba Biblia ( yaani Taurati, Zaburi na Injili) ni neno la ALLAH kama tulivyotibitisha kwa aya mbalimbali za Qurani.

HATIMA:

Maneno ya Allah yaliyokuja katika Biblia yamesalia bila mageuzi au mabadiliko, kama vile kila muisilamu mwenye ujuzi wa kitabu awezavyo kuona. Kwa hivyo ndungu yangu muisilamu unaposema hata sasa kuwa Biblia ( Taurati, Zaburi na Injili) vimechafuliwa na kufanyiwa mabadiliko; kwa maneno mengine unasema hivi:

1. Qurani sio sahihi

Ni wazi kuwa Qurani inatuhakikishia kuwa maneno ya Mola wetu mlezi hayabadiliki ila bado wewe washikilia kuwa Biblia Takatifu imefanyiwa mabadiiko.

2. Allah anadhunishwa

Kwa kuwa unaashilia kuwa ALLAH alishindwa kuyalinda maneno yake, ingawaje Qurani imeshuhudia kwamba hapatakuwa na mabadiliko katika maneno ya Allah.

3. Qurani imefanyiwa mabadiliko

Ikiwa Biblia Takatifu (Yaani Taurati, zaburi na Injili vimewahi kubadilishwa; waeweze kufikria kinachoweza kufanyika kuhusiana na Qurani Takatifu.

Ebu nikuuleze swali ewe ndungu yangu muisilamu , ikiwa kweli iliwezekana Biblia Takatifu kufanyiwa mabadiliko: Je mabadiliko haya yalifanywa lini? Je ilikuwa kabla au baada ya kuja uisilamu? Ikiwa undisi kwa mageuzi haya yalifanywa kabla ya uisilamu; Je inakuwaje basi kwamba Qurani inashuhudia na kuisifu Taurati na Injili? Badala ya mashambulizi kutoka kwa Qurani kuhusu Taurati na Injili hapana chochote ila sifa na kuvitakasa.

Ndungu yangu Muisilamu, sote twaweza kuona wazi kuwa ni yule mtu asiyekuwa na ujuzi wa Qurani tu awezaye kuwa na mawazo kama hayo ; kwani pamekuwepo na ushahidi mwingi wa kuthibitisha kwamba Biblia Takatifu ilikuwepo kabla na hata baada ya kuja ka uisilamu na imebakia vile vile bila mageuzi au mabadiliko.

“Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za mwenyezi Mungu? Q 5:43

Utagundua kwamba kuna tukio la kiajabu lililotokea zamani za Nabii Muhammad ( Tazama Ibn Kathir, uk 517-518).

Inasemekana kwamba kundi la wayahudi walikuja kwa Mtume Muhammmad wakimtaka kuhukumu baina ya wawili mume na mwanamke walioshikwa katika tendo la zinaa. Mtume akawaamuru wairejelee Taurati. Walipojaribu kuificha sehemu iliyotaja kwamba adhabu ya wazinifu ni kuuwawa kwa kupigwa mawe , mtume Muhammad alitambua hiana zao na akawaingiza waifuate Taurati. Hivyo basi wale wazinifu wawili wakapigwa mawe hata kufa.Huu ni ushahidi bayana kwako ndungu yangu muisilamu, kwamba Taurati ilikuwa bado haijachafuliwa wala kufanyiwa mageuzi.

“Sema Enyi watu wa kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlioteremsiwa kutoka na Mola wenu mlezi.”Q 5:68

“Ewe mtume! Waambie watu wa kitabu (yaani Biblia) hakika nyinyi hamtakuwa mnafuata dini sahihi ila mtapo zitangaza hukumu zote za Taurati na Injili ni mkazitenda.”

Tazama Ibn Kathir, uk 535. Utaona kuwa Taurati na Injili sote zilikuwepo sawia na Qurani na bila mabadiliko yeyote.Laiti sivyo, basi Qurani isingeli wataka wayahudi na wakristo wote pamoja, waambatane, waishike na waifuate Taurati na Injili.

“Na wahukumu watu wa Injili kwa yale aliyoteremsha mwenyezi Mungu ndani yake na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha mwenyezi Mungu, basi hao ndio wapotofu.’

Tena tazama Ibn Kathir uk 523 utagundua kwamba Quraniiliwaamurisha wakristo wajihukumu kwa hukumu za Biblia maishani mwao. Litakuwa jambo lisilo wezekana kwa Qurani kuagiza jambo ili ikiwa Biblia yenyewe imefanyiwa mageuzi ya namna yeyote wakati wowote.

“Huwaoni wale waliopewa sehemu ya kitabu? Wanaitwa kukiende kitabu cha mwenyezi Mungu ili kuwahukumu baina yao; kasha baadhi yao wanageuka wanakikataa” Q3:23

Swali la muhimu hapa, ndungu yangu muisilamu ni hili: Inamkinikaje, inawezekanaje kwa Qurani kuwataka Wayahudi wairejee Taurati ili wapate hukumu ya Mumgu ? Lazima sote tukubaliane kwamba haiwezekani jambo ili ikiwa Taurati ingelikuwa kweli imegeuzwa na kwamba mabadiliko haya yalikuwepo hata zamani za uteremsho wa Qurani.

Ukweli kuwa Qurani inawaita wayahudi na wakristo kufuata hukumu za Taurati na Injili mtawalia , ni ishara na ushahidi mwingine kuonyesha kuwa Taurati na injili havijafanyiwa mabadiliko . Mwana historia Al – Badwawi amenakiri kuwa mtume Muhammad alikuwa na mazoea ya kutembelea shule za wayahudi ambamo Taurati ilifundishwa. Wakati mtufulani (Naiem bin Amir) alipomuuliza kuhusu, imani ipi aliyoishika alijibu “Mimi n ijitolea Ibrahimu na Taurati”
“Enyi mliopewa kitabu! Aminini tuliyoyateremsha yenye kusadikisha yale mlio nayo”
Q 4:47

Hapa utaona kuwa Ibn Kathir aliufikia ule uelekevu kwamba Qurani inaiunga mkono Taurati na injili.

“Na aminini ndiyo yateremsha ambayo yanasadikisha ndiyo nayo” Q 2: 41

“Kisha akakujieni mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo” Q 3:81

“Na wanapo ambiwa: Yaaminini aliyo yateremsha mwenyezi Mungu. Wao husema tunaamini tuliyo teremshiwa sisi na kuyakataa yasiyo kuwa hayo. Na hali yakuwa hii ndiyo haki inayo thibitisha yale waliyo nayo wao” Q 2:91

Kwa mara nyingine Ibn Kathir uk 89, utagundua kuwa Qurani inashuhudia ukweli na usafi na usahihi wa Taurati na injili jambo ambalo lisingeli wezekana ikiwa vingekuwa vimechafuliwa.

Pia pana maelezo mengi tofauti tofauti ya mwanawachuoni Ibn Kathir akipeana matukio kadhaa yanayoonyesha jinsi gain mtume Muhammad alivyoenzi na kuvutiwa na Taurati na Injili katika zama zake duniani.

“Na ukiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao kitabu kabla yako.”

Vilevile Al – Baidhawi alihitimshwa pale Qurani iliponakiri “ Na ukiwa unayo shaka (ewe nabii Muhammad) Waulize wale wasomao kitabu kabla yake (yaani wayahudi na wakristo)

Nasi pia twafika hatima hiyo kwamba Taurati na Injili vyote viwili vilijulikana na nabii Muhammad na vilikuwa salama kutokamana na mageuzi na mapinduzi , Natumai sasa, ndungu yangu muisilamu kwamba wakubaliana nami kwamba Taurati na Injili havijawahi fanyiwa machafuko, mageuzi au mapinduzi yoyote yale wakati wowote kabla ya uisilamu, zama za nabii Muhammad wala hata baada ya kuja kwa uisilamu duniani.

HATIMA YA UTAFITI

Taurati na Injili zote zilikuwepo ulimwnguni zamani zile alipokuwa analetewa mtume Muhammad Qurani tukufu na vilikuwepo bila ya mabadiliko ushahidi wa haya ni kama ufuatavyo:

1. Nabii wa Uisilamu (Muhammad) aliwataka Wayahudi wairejeree Taurati iwe kitabu cha kuhukumu baina ya wayahudi (Tazama Q 3:23) Ni wazi kuwa mtume asingeli pendekeza watu wairejeree Taurati na Injili ambavyo vimekorogwa.
2. Qurani inawangaa wayahudi ambao licha ya kutoiamini Quarini walijaribu kuitumia kama hakimu kwao. Niwazi kuwa mtume Muhammad aliwashangaa , na kwa kuwa alikubali Taurati basi aliwataka waitumie Taurati kama hakimu wao, kwani ndani yake mna uongofu na mwelekeo. Q: 47 – 52

3. Kwa kuwa nabii wa uisilamu aliwataka watu wa injili (yaani wakristo) waamini kila kitu kilichokuja ndani yake na waifuate (Qu 5:47) Na wazi pia kuwa mtume Muhammad asingali pendekeza wakristo wakirejeree kitabu kilicho korogwa na kubadilishwa. Huu ni ushahidi tosha wa kuthibitisha kuwa injili ilikuwa safi kipindi cha kuteremshwa Qurani.

4. Wakati Nabii wa uisilamu aliposisitiza ya kwamba wayahudi na wakristo wote waishike Taurati na Injili, kwa kuzingatia hukumu zilizokuja ndani yake (Tazama 54:5 2-52. Je wadhani hata kiufupi tu, kwamba mtume Muhammad angalifanya haya ikiwa Taurati au Injili zingelikuwa zimekorogwa na kubadilishwa?

5. Ukweli ni kwamba Qurani inatupa ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Taurati na Injili view safi na bila dosari yeyote. (Tazama Su 3:81, 5: 47 – 52, 4:47 na Qu 2: 89-91)

6. Qurani ilimshauri mtume wa uisilamu kutafuta msaada kutoka kwa watu wasomao Taurati na Injili wakati wowote akiwa na shaka yeyote katika maswali ya dini. (Ikiwa unayo shaka ewe Muhammad.)hauwezi kamwe kupendekeza kuwa Allah angemshauri mtume wake kwenda kwa watu wenye kitabu kilicho korogwa na kubadilishwa. Au jee waweza kupendekeza kinyume?Je angemrejesha katika Taurati na Injili zilizo badilishwa tayari?

7. Qurani yenyewe inawataka wayahudi na wakristo wawe na imani katika Taurati na Injili.

“Enyi mlio amini !Muaminini mwenyezi Mungu na mtume wake, na kitabu alicho kiteremsha juu ya mtume wake, na kitabu alichokiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa mwenyezi Mungu, na malaika wake, na vita vyake, na mitume wake, na siku ya kiyama, basi huyu amekwisha potelea mbai.” Q 4: 136

Ni jambo la kushangaza na wala haliingi akilini kwamba Qurani itawataka waislamu waiamini Biblia ilyoteremshwa kabla ya Qurani kama Biblia ingelikuwa sio kitabu chenye haki. Huu ni ushahidi kamili wa usafi na ukweli na uhakika wa Biblia, kwani Qurani isingeliwataka waislamu waiamini ikiwa ingelikuwa imebadilishwa na kugeuzwa

Sasa basi ni wazi kwako ndungu yangu muisilamu, baada ya utafiti huu wote na ushahidi huu kutoka kwa Qurani; ni dhahiri na zaidi ya uvuli wowote wa shaka kwamba Taurati na Injili vilihifadhiwa katika zama za kuteremshwa Qurani (kwa kuwa Qurani imetupa ushahidi huo) mageuzi yalifanywa baadaye wakati mwingine.Wacha nikwambie ndungu yangu, kwamba Qurani yenyewe inakanusha jambo hili kwa sababu zifuatazo.

1.Katika Su 5:48 inasaema:
“Na tumekuteremshia wewe wa haki, kitabu hichi nacho sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika vitabu na kuyalinda”

Maana ya “kuyalinda” ni kuwa maandiko ya Mungu yatasalia na kuwa salama kutokamana na mabadiliko na mageuzi na kukologwa.Inamaana wazi kuwa ikiwa Taurati au injili vimebadilishwa baada ya Muhammad au Qurani ni kusema kuwa Qurani ilishindwa katika kazi yake kama “mlinzi” juu ya Taurati na injili kwa maneno mengine ikiwa Taurati na injili vilibadilishwa baada ya kuteremshwa Qurani, basi watu wa Qurani wameshindwa kuhifadhi kulinda na kuchunga angalau nakala moja au zaidi ya Taurati na injili safi kama mlinzi juu yake.

Wakati wakristo walipotambua kwamba Taurati ina aya nyingi zilizomhusu masihi Yesu, walichukua jukumu la kuwa walinzi wake, na wakaisambaza Taurati na injili kote ulimwenguni. Imekadiliwa kuwa Taurati imetafsiriwa karibuni lugha zote zinazo julikana na wanadamu.Kwa nini basi waisilamu hawakufanya kazi kama hii kwani waliamini kuwa Taurati na Injili ilikuwa na aya nyingi tu zinazo mhusu mtume Muhammad na Qurani?

2 Kwa kuwa tayari tumethibithisha ukweli kwamba Taurati na injili vilihifadhiwa safi kutokamana na mageuzi yeyote zamani za uteremsho wa Qurani: basi ili litatupeleka kufikia hatima hii:

3a) Wakristo wa kweli – zamani za uteremsho wa Qurani walihifadhi nakala ya Taurati maana ndani yake mlikuwepo maandiko mengi yaliyomhusu Yesu na injili.Zaidi ya hayo Yesu mwenyewe alishuhudia usafi na uhaki wa Taurati. Pia imenakiriwa ndani ya Qurani:

“Natuka wafuatisha haio Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati , na tukampa injili iliyomo ndani yake uwongofu na nuru na inayo sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachangamfu.’ Q 5:46

Hivyo basi ikiwa kuwa vyovyote vile wayahudi wahgelijaribu kubadilisha Taurati, wakristo wangegundua hilo na kutambua mageuzo hayo mara moja kwani walihifadhi nakala halisi ya Taurati.

b) Vilevile kwa mawazo yaleyale, ikiwa wakristo nao wangeli jaribu kubadili chochote ndani ya Taurati , wayahudi wasingeli



8. Qurani yenyewe inawataka wayahudi na wakristo wawe na imani katika Taurati na Injili.

“Enyi mlio amini !Muaminini mwenyezi Mungu na mtume wake, na kitabu alicho kiteremsha juu ya mtume wake, na kitabu alichokiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa mwenyezi Mungu, na malaika wake, na vita vyake, na mitume wake, na siku ya kiyama, basi huyu amekwisha potelea mbai.” Q 4: 136

Ni jambo la kushangaza na wala haliingi akilini kwamba Qurani itawataka waislamu waiamini Biblia ilyoteremshwa kabla ya Qurani kama Biblia ingelikuwa sio kitabu chenye haki. Huu ni ushahidi kamili wa usafi na ukweli na uhakika wa Biblia, kwani Qurani isingeliwataka waislamu waiamini ikiwa ingelikuwa imebadilishwa na kugeuzwa

Sasa basi ni wazi kwako ndungu yangu muisilamu, baada ya utafiti huu wote na ushahidi huu kutoka kwa Qurani; ni dhahiri na zaidi ya uvuli wowote wa shaka kwamba Taurati na Injili vilihifadhiwa katika zama za kuteremshwa Qurani (kwa kuwa Qurani imetupa ushahidi huo) mageuzi yalifanywa baadaye wakati mwingine.Wacha nikwambie ndungu yangu, kwamba Qurani yenyewe inakanusha jambo hili kwa sababu zifuatazo.

1.Katika Su 5:48 inasaema:
“Na tumekuteremshia wewe wa haki, kitabu hichi nacho sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika vitabu na kuyalinda”

Maana ya “kuyalinda” ni kuwa maandiko ya Mungu yatasalia na kuwa salama kutokamana na mabadiliko na mageuzi na kukologwa.Inamaana wazi kuwa ikiwa Taurati au injili vimebadilishwa baada ya Muhammad au Qurani ni kusema kuwa Qurani ilishindwa katika kazi yake kama “mlinzi” juu ya Taurati na injili kwa maneno mengine ikiwa Taurati na injili vilibadilishwa baada ya kuteremshwa Qurani, basi watu wa Qurani wameshindwa kuhifadhi kulinda na kuchunga angalau nakala moja au zaidi ya Taurati na injili safi kama mlinzi juu yake.

Wakati wakristo walipotambua kwamba Taurati ina aya nyingi zilizomhusu masihi Yesu, walichukua jukumu la kuwa walinzi wake, na wakaisambaza Taurati na injili kote ulimwenguni. Imekadiliwa kuwa Taurati imetafsiriwa karibuni lugha zote zinazo julikana na wanadamu.Kwa nini basi waisilamu hawakufanya kazi kama hii kwani waliamini kuwa Taurati na Injili ilikuwa na aya nyingi tu zinazo mhusu mtume Muhammad na Qurani?

2 Kwa kuwa tayari tumethibithisha ukweli kwamba Taurati na injili vilihifadhiwa safi kutokamana na mageuzi yeyote zamani za uteremsho wa Qurani: basi ili litatupeleka kufikia hatima hii:

3a) Wakristo wa kweli – zamani za uteremsho wa Qurani walihifadhi nakala ya Taurati maana ndani yake mlikuwepo maandiko mengi yaliyomhusu Yesu na injili.Zaidi ya hayo Yesu mwenyewe alishuhudia usafi na uhaki wa Taurati. Pia imenakiriwa ndani ya Qurani:

“Natuka wafuatisha haio Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati , na tukampa injili iliyomo ndani yake uwongofu na nuru na inayo sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachangamfu.’ Q 5:46

Hivyo basi ikiwa kuwa vyovyote vile wayahudi wahgelijaribu kubadilisha Taurati, wakristo wangegundua hilo na kutambua mageuzo hayo mara moja kwani walihifadhi nakala halisi ya Taurati.

b) Vilevile kwa mawazo yaleyale, ikiwa wakristo nao wangeli jaribu kubadili chochote ndani ya Taurati , wayahudi wasingeli kubali na wangewazuia mara moja kwa tendo la kuleta nakala halisi ya Taurati.

c) Vilevile, kama wayahudi wangelijaribu kubadilisha injili, wakristo wangali wazima kwa kuileta nakala safi na halisi ya injili.

4. Ni –bayana kuwa uisilamu asilia kama ulivyo, umekuja karibuni miaka 570 baada ya ukristo. Wakati wa kabla ya uisilam, zama za ujinga, ukristo ulikuwa umezaenea takriban kote ulimwenguni ikiwemo Afrika , uabeshi, Irani, India na Uropa.

Hii ilipelekea ugumu kwa watu wa sehemu moja ulimwenguni kubadilisha injili kuwa kazi nzito na isiyo wezekana.

5. Na sasa ndungu yangu muisilamu, lazima tujiulize wenyewe basi: Ni lini ni wapi mageuzi hayo yalifanywa? Ni nani aliyeyafanya mageuzi hayo?Hakuna yeyote ambaye anaweza kutoa na kuthibithisha jina hata moja tu la mwana historia. Myahudi au mkristo anayeweza kudhihirisha jambo hilo.Tena kama basi mageuzi na mabadiliko yeyote yalifanywa kwa makubaliano ya makundi yote mawili, wayahudi na wakristo; basi itakuwa ina maana pana mgongano, kwani Qurani inashuhudia kwamba – Hapana mabadiliko katika maneno ya Allah.

“Nasoma uliyofunuliwa katika kitabu cha Mola wako mlezi. Hapana awezaye kubadilisha maneno haya.”Q 18 :27

Hapana shaka kwamba neno “kitabu” lililotajwa katika ayah ii inaashiria Qurani lakini tamko Maneno yake” Yanaashiria Biblia Takatifu (Yaani Taurati, Zaburi na injili). Vitabu hivi vyote ni maneno ya Allah na tunaamini hapana yeyote awezaye kubadilisha maneno yake.

“Hapana mabadiliko katika maneno ya mwenyeziMungu.” Q 10:64

“Na hakuna abadilishaye maneno ya mwenyezi Mungu.”

HITIMISHO:

1. Biblia (Taurati, zaburi na injili) ni neno la Allah alilopeana Allah kwa waja wake, mitume kabla yenu injili ni mwongozo, nuru na rehema kwa ulimwengu.
2. Qurani anajenga usawa baina yake na Biblia (Yaani Taurati, Zaburi na Injili) kwani zote zililetwa na Allah kwa wajumbe wake kabla yenu.
3. Qurani inajipa jina la sifa kama lile lile inaloipa Biblia – Yaani “kitabu”
4. Maneno ya Allah yaliyopeanwa kwa wajumbe wake yalisalia hivyo na wala bado hayajafanyiwa mabadiliko

“Hakika sisi ndio tulioteremsha ukumbusho huu na hakika sisi ndio tutao ulinda” Q 15 : 9
5. Biblia Takatifu ilikuwepo kipindi ambapo Qurani inateremshwa. Ushahidi ni kuwa , mtume Muhammad aliwataka wayahudi wailete Taurati kuwa hakimu katika mjadhalo baina yao.
6. Ni jambo la kustaajabisha kudhai kuwa kitabu chochote katika vitabu vitakatifu vya mwenyezi Mungu mlezi viliwahi kufanyiwa mabadiliko kwani ukweli ni kwamba Taurati na injili vilikuwa vimekwisha tapakaa kote ulimwenguni katika lugha mbali mbali.

NDUNGU YANGU MUISILAMU:

Utafiti huu wote unaungwa mkono na maandiko na dalili kutoka kwa Qurani na pia unaungwa mkono na mabingwa miongoni mwa wanavyuoni wakubwa w kiislamu kama vile Ibn Kathir, Al – Baidhwawi, Al – jalaleen na Al – Bukhari.

Nimeenda umbali huu wote ili kumfanya kila muisilamu wa kweli atosheke kuwa utafiti huu ulifanywa katika uwazi na ukweli. Nimekuwa mwangalifu kutumia Qurani kama haswa kitabu rejeshi ili kukuhakikishia kwamba, wakati utakapokuwa umehitimisha kusoma utafiti huu ,utaweza kukubaliana nami kuwa, Biblia Takatifu (Yaani Taurati, zaburi na injili) vimehifadhiwa kutokamana na mageuzo yeyote au mabadiliko yeyote. Hivi vyote ni vitabu vya Allah nani maneno yake, na tunaamini hakuna yeyote awezaye kubadilisha maneno ya mwenyezi Mungu.

“ Hapana mabadiliko katika maneno ya mwenyezi Mungu” Q 10:64

“Hakika sisi ndio tulio teremsha ukumbusho huu, na hakika sisi ndio tutaolinda.” Q 15:9

Ndungu yangu muisilamu, ikiwa una maswali yeyote kuhusu haya niliyoandika au ikiwa unatamani kupata nakala yako ya Biblia Takatifu, tafadhali niandikie kwa anwani zifuatazo:

Al Shaikh Muhammad Kamal