Wednesday, December 8, 2010

JE ISA BIN MARYAMU NDIYE YESU KRISTO?

JE , ISA BIN MARYAMU NDIYE YESU KRISTO?

Utangulizi

Kwa miaka mingi sasa imekuwa ni kawaida kuwasikia Waislamu wakifundisha jamii kuwa Isa bin Maryamu” kama Qurani inavyofundisha ndiye “Yesu Kristo”. Mafundisho haya Hivi sasa yanaendeshwa kwa mtindo wa kulinganisha aya za Biblia na Qurani. Wahadhiri wa dini ya kiislamu wanaendesha Mihadhara ambayo imeenea sana duniani na hasa zaidi katika nchi za Africa ya Mashariki na Kati (East and Central Africa). Wahadhiri hao pia huchapisha vijarinda na kurekodi kanda(Cassette) za Audio na Video, ambazo zimesababisha baadhi ya Wakristo waamini kuwa Isa Bin Maryamu ndiye Yesu Kristo. Swali la msingi kwa Wakristo wote; Je, ni kweli kuwa Isa bin Maryamu ndiye Yesu Kristo? Nakusihi fuatilia somo hili ili kujua ukweli.

SEHEMU KUU NANE ZA SOMO HILI

  1. Hoja zinazotumika na Waislamu kusema Isa ndiye Yesu.
  2. Je,Mama wa Isa ndiye wa Yesu?
  3. Maana ya jina Isa

4. Maana ya jina Yesu

  1. Je,kuzaliwa kwa Yesu ni sawa na Isa?

6. Je,Isa bin Mariam ni Mwana wa Mungu?

7. Je,Mamlaka ya Isa na Yesu ni sawa

8. Ikiwa Yesu ndiye Isa je, Isa alikufa?

9. Ujue umuhimu wa kumuamini Bwana Yesu


1.Hoja zinazotumika na waislamu kusema Isa ndiye Yesu.


1.Hoja ya kwanza – Mama wa Isa jina lake Maryamu

Qurani 3:45 Suratul Aal-Imran (watu wa Imran)

(Kumbukeni)waliposema malaika, “Ewe Maryamu Mwenyenzi Mungu anakupa habari njema za (kumzaa mtoto bila mume bali kwa kutamka] Neno tu litokalo kwake (la kumwambia zaa ukazaa pasina kuingiliwa) jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na ahera na miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyenzi Mungu

Marko 6:3-4

Huyo si yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake na nyumbani mwake.

Hapa Waislamu wanasema kama vile Qurani inavyofundisha jina la Mama wa Isa ni Mariamu kadharika Biblia inafundisha jina la Mama yake Yesu ni Maryamu. Hivyo wanasema kuwa Yesu ndiye Isa. Soma pia Mathayo 1: 18-21 na Yohana 2:1

2.Hoja ya pili Isa ni Mtume wa Allah kwa Waisraeli

Quran 4:171 Suratul An Nisaa (Wanawake)

Enyi watu wa kitabu msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo kweli. Masihi Isa bin Maryamu ni mtume wa Mwenyenzi Mungu…

Hapa tunaona kuwa Qurani imemtaja Isa kuwa ni Mtume, je, mtume kwa akina nani? Endelea kusoma aya hii katika Qurani.

Quran 61:6 Suratul As Saff [Msitari wa vita/Wajipangao safusafu]

Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad...Soma pia katika Quran 3:49 Suratul Aal Imran

Aya hii inathibitisha kuwa Isa ni mtume kwa Waisraeli. Je, Yesu ni mtume kwa akina nani?

Waislamu wanaoendesha mihadhara pia husoma aya hizi za Biblia

Waebrania 3:1

Kwa hiyo ndugu watakatifu wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtakafarini sana mtume na kuhani mkuu wa maungamo yetu Yesu.

Mathayo 15:24

Akajibu, akasema, “Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli”

Kwa hivyo kama Quran inavyofundisha kuwa Isa mwana wa Maryamu ni mtume kwa Waisraeli ndivyo Biblia inafundisha kuwa Yesu ni mtume kwa waisraeli hivyo basi Isa ndiye Yesu. Hivi ndivyo wahadhiri wa dini ya Uislamu wanavyoifundisha jamii. Je, hoja hii ni sahihi nitajibu huko mbele:-

3.Hoja ya tatu

Isa bin Maryamu alifanya miujiza

Qurani 5:110 Suratul Al Maidah (Meza)

(kumbukani tena) mwenyenzi Mungu atakaposema ,Ewe Isa mwan wa MaryamuKumbukeni neema yangu juu ya mama yako.Nilipokusaidia kwa [kukupa kuwa na wewe ]Roho takatifu[Jibrili],ukazungumza na watu [maneno ya nafuu]katika utoto[wako] na katika utu-uzima [wako].Na [kumbuka].Nilipokufundisha kuandika na [nikakupa] hikima,Taurati na Injli na ulipotengeneza kwa udongo sura za ndege kwa idhini yangu,na ulipo waponesha vipofu na wenye mbalanga kwa idhini yangu,na ulipowatoa [baadhi ya] wafu [makaburi mwao] kwa idhini yangu,na Nilipokuzuilia wana wa Israili [wasikudhuru] ulipowafikia kwa hoja zilizo wazi;wale walio kufuru miongoni mwao wakasema:Haya si chochote ila ni uchawi dhahiri.

Waislamu wanasema huu ni ushahidi wakutosha kwani Allah anasema Isa alifanya miujiza mingi hii.

Isa aliponyesha vipovu ndiye …………….. Yesu aliponyesha vipovu Marko 10:46-52

Aliwafufua wafu makaburi ndiye………….. Yesu alifufua wafu Marko 5:21-43

Aliwaponyesha wenye mbalanga Ndiye…... Yesu aliponya Ukoma Luka 17:1

Wahadhiri wa kiislamu wanasema kama vile Qurani inavyosimulia kuwa Isa amefanya miujiza mingi, ndivyo Biblia inavyofundisha hivyo Yesu ndiye Isa isitoshe wanasema hivi:-

Isa bin Maryamu ni Nabii, Suratul An- Nisaa 4;171, kadhalika Biblia inafundisha kuwa Yesu ni Nabii, Yohana 6:14, Yohana 7:40, Luka 13:33,Luka 24:19, Marko 6:4 na Mathayo 13:57. kwa wastani Biblia inafundisha kuwa Yesu ni Nabii mara 12. Vile vile wahadhiri wa Kiislamu wanafundisha ya kwamba Isa ni Neno la Kiarabu ,katika kiingereza Jesus na kwa Kiswahili niYesu.Kupita vigezo hivi baadhi ya Wakristo wameshawishika kuamini kuwa Isa ndiye Yesu. Lakini, lazima tuzichunguze hizi hoja moja baada ya nyingine ili tujue ukweli.

2.Je,Mama wa Isa ndiye wa Yesu Kristo?

Hapo awali tumeona kuwa Mama wa Isa anaitwa Maryamu, Suratul Al Imran 3:45 na pia Mama wa Yesu anaitwa Mariamu Mathayo 1:18-21, Marko 6:3-4 lakini kufanana kwa majina hakuwezi kamwe kumaanisha kuwa ni mtu mmoja. kwani walio na Jina hilo ni wengi. Biblia inatufundisha hivi.

Yohana 19:25

Na penye Msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama, Mamaye, na umbu la Mamaye M ariamu wa Klopa na Mariamu Magdalena.

Hapa tunaona Mariamu watatu. Ili kutambua tofauti baina ya Mariamu Mama wa Isa na Mama wa Yesu, lazima tulinganishe ujumbe wa Qurani na Biblia. Qurani inasimulia kuhusu Baba na Kaka wa Mariamu Mama wa Isa hivi.

Suratul Al Tahrym 66:12 [kuharimisha]

Na Maryamu mtoto wa Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na tukampuliza humo roho yetu, (inayotokana na sisi) na akayasadikisha maneno ya mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa)

Surah Al-Maryam 19:28

Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati.

Hapa tunaona kuwa Maryam Mama wa Isa Baba yake ni Imrani na Kaka yake aliitwa Haruni.

Tusomapo Biblia inatueleza kuwa Amrani aliwazaa hawa.

Hesabu 26:59

Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa lawi ,ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri;na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni,na Musa,na Miriamu umbu lao.

Soma pia 1 Nyakati 6:1-3 na Kutoka 6:20

Huyo Amrani aliishi miaka mingi Kabla ya Yesu na, tena ametokana na kizazi cha Lawi mtoto wa tatu wa mzee Yakobo. Mwanzo 29:34 Kut. 2:1-10. Ikiwa Mariamu wa Qurami Baba yake ni Imrani basi atakuwa ameishi miaka 1500 kabla Mama yake Yesu hajazaliwa!

Je, Mariamu mama wa Yesu ametokana na kizazi gani?

Tunaposoma Biblia tunaona kwamba Yesu anaitwa mwana wa Daudi Mathayo 1:1 Marko 10:47 na Luka 1:27,32 ndio maana pia Yesu anaitwa Simba wa Yuda Ufunuo 5:5. Hivyo basi ukoo aliyetoka Yusufu na Mariamu Mama wa Yesu ni mmoja.

3.Maana ya Jina Isa.

Ni jambo la kawaida sana jina au majina kuwa na maana. Mfano majina haya ya kiarabu yana maana hizi. Muhammad linaamanisha mwenye kushukuriwa, Abdallah ni Mtumwa wa Allah Abu-Bakar maana yake ni Baba wa bikira, Abu Huraira ni Baba wa mapaka.

Aidha majina ya Kiebrania nayo pia yana maana. Malaki ni mtumishi au Mjumbe wa Yehova, Isaya ni Wokovu wa Yehova, Ezekiel inaamanisha Mungu hutia nguvu, Daniel Mungu ni Hakimu wangu.

Jina Isa maana yake ni hii.

Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30 Surah 114 aya 6236 maneno yenye kutamkika 76,440 herufi 322,373 jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa na Imam Baidawi voI.1 ukurasa wa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe.

4.Maana ya jina Yesu

Jina Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘Iesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema “ Yasu.”kwa kiingereza ni ‘’Jesus’’ Maana yake “Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi”Soma aya hizi..

Mathayo 1:18-21 na Luka 2:8-11. Bwana maana yake Mungu ndiye mwokozi Isaya 43:6, 10-11. Katika Biblia ambayo ina jumla ya Surah 1189 aya 31,102 vitabu 66 39, Agano la kale na 27 agano jipya neno Mwokozi kiiengereza wanasema Saviour limetajwa mara 55. ikumbuke kwamba katika agano jipya jina Yesu au kiebrania Yehoshua kiarabu Yashua au Yasu limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226. zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na Sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa siyo Bwana Yesu.

5Je,kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni sawa na Isa?

1.Taarifa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.

Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa

Gabrieli alivyomtokea Mama wa Yesu

Alienda kwa Mariamu aliyekuwa msikitini Qurani 19:16-17 Saratul Mariam

  1. Alienda kwa Mariamu aliyekuwa Nyumbani kwake .Luka 1:26-28

  1. Mariamu Mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji gani wala mji gani wala hata nchi haijulikani. Isitoshe Qurani inasema kuwa Jibrili ndiye aliyemleta utume Muhammed asiwapelekee Mayahudi (hana kosa),Soma Qurani 2:97 Suratul Al-Baqarah

  1. lakini Mariamu Mama yake Yesu alitokewa na malaika Gabrieli akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya Israel Luka 1:26

Mariamu Mama wa Yesu ni Myahudi.

2.Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu Mama wa Isa ila alijimithilisha kwa umbo la binadamu aliye kamili Qurani 19:7 Suratul Mariam

  1. Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu Luka 1:28.

  1. Jibrili alimwambia Mariamu kwamba mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe Mwana Mtakatifu Qurani 19:19 Suratul Mariam

  1. Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye mtoto muujiza kwa wanadamu QuranI 19:21Suratul Mariam. Isitoshe Jibrili hakutaja jina la Mwana kwa Mariamu. Bali alisema ili nikupe Mwana Mtakatifu.

  1. Lakini malaika Gabrieli alimwambia Mama waYesu kuwa utachukua mimba Luka 1:31

5. Malaika Gabrieli alisema kwa Mariamu Mama wa Yesu kuwa mtoto jina lake utamwita Yesu Luka 1:31, 2:21 Gabrieli hakusema kuwa atampa Mwana Mariamu. Bali alisema Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani mtoto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.

2.Tofauti ya kuzaliwa kwa Isa na Yesu ni hii.

Isa bin Mariam.

Yesu Kristo.

  1. Isa alizaliwa katika shina la mtende Qurani 19:23 Suratul Mariam.

  1. Yesu kazaliwa katika hori la kulishia ng’ombe Luka 2:7

  1. Kuzaliwa kwa Isa haijulikani kama mimba ya mama yake ilichua muda gani maana malaika Jibrili alisema nikupe mwana mtakatifu mara akachukua mimba na kuzaa Qurani 19:22-23 Suratul Mariam.

  1. Lakini Mariamu Mama wa Yesu siku zake za kuzaa zilitimia Luka 2:6-7

3.Qurani haionyeshi kama Isa alitabiriwa na manabii kuwa atazaliwa

  1. Lakini Biblia inatuthibitishia kuwa manabii walitabili kuzaliwa kwa Yesu, Isaya 7:14, 9:6 utabili huu ulitolewa na Nabii Isaya miaka 750 kabla ya Yesu kuja kuzaliwa nao ulitimia Mathayo 1:18-23

  1. Isa haijulikani alizaliwa katika kijiji gani wala mji, wala nchi aliyozaliwa Qurani haikueleza.

4. Biblia inatujulisha kuwa Yesu alizaliwa Bethelehemu ya Uyahudi katika Mji wa Daudi umbali wa maili 5 toka kusini mwa Yerusalemu nchi ya israel Tazama Luka 2:8-16. Kuzaliwa kwake mahali hapo pia ni kutimiza unabii uliotowe na Nabii Mika miaka 750-686 kabla ya kristo kuja wakati wa wafalme – hawa wakitawala – Jotham, Ahaz na Hezekia wafalme wa Yuda. Yesu mwenyewe alizaliwa kama mwaka wa 4 wakati wa Mfalme Herode Mkuu akitawala Yuda tangu

  1. Isa aliongea na watu akiwa mtoto mchanga, na kusema kuwa yeye ni mja wa Mungu amepewa kitabu na amefanywa Nabii Qurani 19:30-33 Suratul Mariam.

  1. Yesu hakuongea na mtu akiwa mtoto mchanga. Alianza kuwauliza maswali na kutoa majibu akiwa na wazee Hekaluni akiwa na miaka 12 Luka 2:42-49.

Hivyo tunaona kwamba kuna tofauti nyingi tu kati ya Bwana Yesu na Isa.Swali kwako mfuatiliaji je, Isa bin Maryamu ndiye Bwana Yesu Mwokozi? Tafakari.

6.Je,Isa bin Mariam ni Mwana wa Mungu

Kama kuna jambo ambalo Allah Mungu anayeabudiwa na waislamu analikataa sana kupitia Qurani basi jambo hilo si lingine bali ni uwana wa Mungu. Allah anasema hivi.

Quani 6:101 Suratul Al-An-am [Wanyama]

Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. inamkinikanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu.

Qurani 9:30 Suratul At-Tawba [Kutubu]

Na mayahudi wanasema “uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu;”na “Wakristo wanasema Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasina na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyenzi Mungu uwaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!

Hili ni agizo la kutisha kwamba Wakristo na Wayahudi tuangamizwe kwa kuwa tumaamini Mungu ana Mwana au wana, lakini Wakristo tunaoamini hivyo kwa sababu Mungu wetu

1.Yehova alifundisha kuhusu Bwana Yesu hivi:

Kutoka 4:22 … Israeli ni mwanangu mimi...

Mathayo 17:5 ….Huyu ni mwanangu mpendwa wangu…

2.Malaika wa Mungu alisema hivi.

Luka 1:30-31,35

Malaika akamwambia usiogope Mariamu,kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume;na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia,Roho Mtakatifu atakujilia juu yako,na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.

Hivyo Isa siyo Mwana Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa.

7.Je,Mamlaka ya Yesu ni sawa Isa? .

1.Qurani inasimulia kuhusu Isa bin Maryamu hivi.

Qurani 5;75 Suratul Al Maidah (Meza)

Masihi bin Maryamu “si chochote ila mtume (tu).” (Na) bila shaka mitume wengi wamepita kabla yake (Hawajaona?) na mamake ni mwanamke mkweli (na) wote wawili walikuwa wakila chakula (na kwenda choo. Basi waungu gani wanaokula na kwenda choo?) Tazama jinsi tunavyo wabainishia aya, kisha tazama jinsi wanavyogeuzwa (kuacha haki).

Hapa tunaona Qurani inasimulia kuwa masihi Isa si chochote ila mtume tu.Hivyo hana Mamlaka. .

2.Mamlaka ya Bwana Yesu ni haya.

Mathayo 28:18

Yesu akaja kwao akasema nao akawambia, “nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

Malaika Gabrieli alisema hivi.

Luka 1:30-33

Malaika akamwambia, “Usiogope Mariamu kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama utachukuwa mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyu atakuwa mkuu ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele na ufalme wake utakuwa hauna mwisho

Bwana Yesu mwenye alisema hivi.

Yohana 17:1-2

Maneno hayo aliyasema Yesu;akainua mikono yake kuelekea mbinguni,akasema,Baba saa imekwisha kufika Mtukuze mwanao,ili Mwana wako naye akutukuze wewe;kama vile ulivyompa Mamlaka juu ya wote wenye mwili,ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele

Warumi 14:9

Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii awamiliki waliokufa na walio hai pia.

Hivyo basi Yesu ana mamlaka kwa watu wote wenye mwili na pia ni mfalme wa milele.

8.Ikiwa Yesu ndiye Isa je,Isa alikufa?

Jambo moja lenye kuleta utata miongoni mwa waislamu ni kuhusu kufa kwa Isa .Waislamu wa jumuiya ya Ahamadia wao wana amini kuwa Isa alikufa kifo cha kawaida kule India na siyo msalabani. lakini waislamu wa madhehebu ya Suni,Shia,Shafi, na mengineyo wanaamini kuwa Isa bin Maryamu hajakufa wakinukuu aya hii…

Qurani 4:157-158 Suratul An-Nisaa (Wanawake)

Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima.

Aya hii inasimilia kuwa Isa hawakumuua wala hawakumsulubu lakini ukianza kusoma aya ya

156 inasimulia hiv...

Qurani 4:156 Suratul AnNisaa (Wanawake]

Na kwa sababu ya kufukuru zao na kumzingizia Maryamu uwongo mkubwa (kuwa kamzaa nabii Isa kwa kuzini)

Hiki ni kisa cha kuhusu kuzaliwa kwa Isa, yaani dhama za utotoni ndio maana aya zinazofuatia zinasema hawakumua. lakini tukiendelea kusoma aya nyingine inasimulia hivi.

Qurani 21:7-8 Suratul Al Anbiyaa (Manabii)

Hatukuwatuma (hatuwapa utume) kabla yako ila wanaume (wa kibinadamu, si malaika) tiliowafunulia (tuliowaletea wahyi). Basi waulizeni wenye kumbukumbu (ya mambo ya zamani) ikiwa nyinyi hamjui. Wala hatukuwajalia (hao mitume kuwa] miili isiyo kula chakula, wala hawakuwa wenye kukaa milele(wasife).

Qurani 21:34 Suratul Al Anbiyaa

Nasi hatukumfanya mwanadamu yeyote kabla yako aishi milele.Basi ukifa wewe, wao wataishi milele?

Aidha Qurani inasema mitume waliokuja na hoja zilizo wazi wazi waliuwa Qurani 3:183 kadiri ya Qurani hiyo hiyo Isa alikuja na hoja waziwazi tazama Qurani 5:110

Isa mwenyewe alitabili mambo makuu matatu haya...

Qurani 19:33 Suratul maryamu

Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa na siku nitakayo kufa na siku nitakayofufuka kuwa hai.

Lipo fundisho kuwa Isa atarudi tena duniani aoe, azae watoto,ndipo afe harafu afufuliwe. Lakini fundisho hili ni dhana tu. Hakuna aya yoyote katika Qurani inayofundisha hivyo. Kumbuka Qurani inasema, “hatukufanya mwanadamu yeyote kabla ya Muhammad aishi milele asife kufa. Swali Je, Isa ni mwanadamu au la? Na je, ikiwa ndivyo aliishi kabla ya Muhammad au baada ya Muhammad? Vyovyote ilivyo iwe Isa amekufa au hakufa bado Isa siyo Yesu.

Bwana Yesu alisulubiwa na kufa na kufufuka siku ya tatu.

Yohana 19:18,33

Wakamsulibisha huko,na wengine wawili pamoja,mmoja huku na mmoja huku, naYesu katikati. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa,hawakumvunja miguu.

Mathayo 28:5-6

Malaika akajibu,akawaambia wale wanawake,Msiogope ninyi;kwa maana najua yakuwa mnamtafuta Yesu aliyesubiwa. Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema.Njoni,mpatazame mahali alipolazwa.

Aya hizi zote zinatudhibitishia kuwa Bwana Yesu alikufa na kufufuka.Hivyo Isa siyo Yesu.

9. Ujue umuhimu wa kumwamini Bwana Yesu

Baada ya kujifunza kwa urefu kuhusu tofauti kubwa kati ya Isa na Bwana Yesu. Na kugundua kuwa Isa siyo Bwana Yesu hata kidogo. Pengine sasa unaweza kubaki na mawazo kuwa huyu Isa mbona Qurani inamwita Nabii! tena inasema ni mtume. Tazama Qurani 19:33 na 61:6. Pia Isa kapewa injli Qurani 57:27.Je, kwa nini nisimwamini? Tukisoma Biblia inayotuongoza Wakristo haitupasi kushtuuka na kuamini tu ili mradi mtu ameitwa mtume au nabii, jambo kubwa ni kupima huo utume wake au huo unabii wake, je umetokana na nani? Tukiongozwa na aya hii…

1Yohana 4:1

wapenzi misiiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu. Kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.

Bwana Yesu alituonya kuwa watatokea manabii wa uongo Mathayo 24:24. Nao tutawatambua kwa matunda yao, Yaani mafundisho.

kuhusu Mitume Biblia inatufundisha hivi...

2 Wakorintho 11:13-14

Maana watu kama hao ni mitume wa uongo watendao kazi kwa hila,wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.Wala si ajabu.Maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Majibu kuhusu hoja ya kusema Isa kapewa injili ni haya…

Wagalatia 1:6-9

nastaajabu kwa kuwa mmemwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kuigeukia injili ya namna nyingine.Wala si nyingine;lakini wapo watu wawatabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa ni sisi au Malaika wa mbinguni akiwahubiria ninyi injili yeyote isipokuwa hiyo mliyoipokea na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiria ninyi injili yeyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.

Kadiri ya Biblia injili ya kweli ni ile inayofundisha ya kuwa.Yesu alikufa,na kufufuka ili atuokoe.Injili isiofundisha hivyo ni ya uongo.Tafakari kuhusu Isa!

Kumfuata Yesu kuna umuhimu mkubwa maana Yesu mwenyewe anasema hivi…

Yohana 14:6

Yesu akamwambia,Mimi ndimi njia,na kweli,na uzima mtu haji kwa Baba,ila kwa njia ya mimi.

Isitoshe Bwana Yesu ndiye atakayemlipa kila mtu.

2 Wakorintho 5:10

kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyoyatenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mabaya au mema.

Ikumbukwe kuwa Isa bin Maryamu hana sifa hizi hata moja kadiri ya Qurani. Hivyo basi ninategemea umeweza kujua kuwa, Isa bin Maryamu siyo Bwana Yesu hata kidogo.

Nimatuimaini yangu kuwa utafikisha ujumbe huu kwa watu wa mataifa ili wamwamini Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo,ili waokolewe. Bwana akubariki sana.

Ni mimi katika utumishi wa Bwana Yesu

MWALIMU

Onyo! Hairusiwi kutoa copy ya somo hili.

16 comments:

  1. nice to write that Jesus is our God,Iam happy toget this

    ReplyDelete
  2. Mi nikuulize mwalimu..mbona munatuchanganya hamtufundishi maandiko yote kwa usahihi wake...nani ataamini kuwa mungu yesu kazaliwa kwenye zizi la ng'ombe ...hana thamani,..pia kama yesu ni mungu mbona hakujiokoa kutoka msalabani...quran tangu ishuke hadi leo haijabadilika hata herufi moja lakini biblia mbona kuna agano jipya na la kale...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ujinga, aliyekwambia quran ilishuka alikudanganya, hayo ni mawazo ya watu yenye uvuvio wa mungu wao(alah) ambaye SIYE MUNGU WA IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO(ISRAEL), Mungu aliyemtoa mwanae wa pekee ili kila mtu amwaminie asipotee bali awe na uzima.

      Delete
    2. Bwana Yesu alikuja kukamilisha yaleeee yaliyotabiriwa kwamba atakufa msalabani na atafufuka siku ya tatu na ndio maana siku wanaenda kumshika alijua. na pia alimponya aliyekatwa sikio alipokuwa anamtete Yesu asichukuliwe na maaskari. hayo yote ni ili yatimie yaliyonenwa na manabii. (pia unajua ni kwa nini aliwaacha wamuue??!! ni kwa sababu yako wewe na mimi ili atuokoe kutokana na dhambi maana alibeba rahana na dhambi zetu ili tukombolewe.

      Delete
    3. Sasa ndugu sikia kujiokoa alikuwa na uwezo wote ila alikuja duniani kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu Ili ukombozi upatikane la uhai utoke yaani damu mfano rahisi ukoloni barani afrika Ili watu wjikomboe ilitakiwa damu n ivyo basi alikuja iliafe sasa sasa atajizuiaje tena??

      Delete
  3. Mi nikuulize mwalimu..mbona munatuchanganya hamtufundishi maandiko yote kwa usahihi wake...nani ataamini kuwa mungu yesu kazaliwa kwenye zizi la ng'ombe ...hana thamani,..pia kama yesu ni mungu mbona hakujiokoa kutoka msalabani...quran tangu ishuke hadi leo haijabadilika hata herufi moja lakini biblia mbona kuna agano jipya na la kale...

    ReplyDelete
  4. Mwalimu gani unarukaruka hoja? Sasa hapo mi sijaelewa umefundisha nini cz hakuna tofauti ya yesu na issa bt Yesu wa waislam ni mtukufu zaidi kuliko huyo wa kwenye biblia! Hata wewe unalijua hilo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. weeee usimlinganishe bwana wa mabwana na isa ni vitu viwili tofauti kabisa hivyo. na usipomkiri Yesu kwa kinywa chako umepotea, na ndipo mtihani unapokuja kwenu nyie waislam mnajifanya mnamjua lakini hamumkiri na ndo maana Bible inasema kila ulimi utakiri kuwa mimi ni bwana. ahaaaaaa.... na ndivyo mnavyofanya. nyie subilini mabikira 75 mliahidiwa. ila kwa upande wetu tumeahidiwa uzima wa milele. karibu kwa Yesu ule raha

      Delete
  5. roho ya mpinga Kristo(alah) ilianza kutenda kazi tangu siku za KRISTO mwenyewe na tangu miaka ya 600 AD, ndo ilitenda kazi kwa kasi kubwa sana na hata sasa pia.
    Misiwashangai hao jamaa,shetani yuko kazini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakushangaa usojielewa atahujui maana ya mpinga kristo ni na Historia yake ni ipi. Katuteni utafiti naona mwalimu wa hii mada kapotosha maandiko ya Quran na hakufanya utafiti ya kina katika Qurani bali aliengemea upande mmoja wa mada.

      Delete
  6. Alah ndiye shetani mkuu! Haina haja ya kubishana na watu wenye uelewa mdogo! Qurani yenyewe inajichanganya kweli kweli maana ni maneno ya uzushi Ya lucifer!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naona Wakristo wako na akili finyu kwa sababu hawasomi maandiko. Unadai Allah ni Shetani. Wewe hujijui jichunguze utapata wewe ndio shetani

      Delete
  7. Inshalah allah awape muongozo wote walopotea na waweze siku moja kushahadia ili wapate janaaaa mi kwangu dua inatosha

    ReplyDelete
    Replies
    1. pia usubili mabikira 75 kama mlivyoahidiwa na alla (mungu mwezi) mnachowaza nyie ndugu zetu ni uzinzi tu kama mtume wenu alivyokuwa yaani alivyowaridhisha na ndo maana akaweka shariah ya kuoa wake wengi sababu alikuwa na tamaa ili ahiridhishe tamaa yake ya kimwili njoo kwa Yesu ule raha wewe.

      Delete
  8. waislamu ni wabishi sijawahi oba

    ReplyDelete
  9. Ukristo ni kichwa cha mwendawazimu.

    ReplyDelete